Damu yaweza Kuokoaje Uhai Wako?
Utiaji damu mishipani umesifiwa sana kuwa utaratibu salama, wenye kuokoa uhai. Lakini Dkt. Alan A. Waldman aeleza hivi: “[Ule] ufahamu wenye utulivu wa kadiri juu ya usalama wa vitu vifanyizwavyo kwa damu ulibadilishwa kiajabu wakati UKIMWI wenye kuhusiana na kutiwa damu mishipani ulipogunduliwa.”
Hata hivyo UKIMWI sio tu hatari iliyopo. “Matukio mengine kadhaa yamechangia ile hisia ya kwamba kuna hatari zisizojulikana na zisizodhibitiwa kwa utumizi wa damu iliyochangwa,” Dkt. Waldman aonyesha wazi. “Sasa, hata mambo yaliyokuwa yakichukuliwa kuwa yametatuliwa—kwa kielelezo, matokeo ya kufanya uchunguzi wa wabebao kiini cha hepataitisi B—yametiliwa shaka.”—Diagnostics & Clinical Testing, Julai 1989.
Kweli kweli, damu ni kitu hatari. Wakati ule ule, damu ni muhimu ili kuokoa uhai. Damu yaweza kuokoaje uhai wako? Utanufaika kutokana na uchunguzi wa swali hilo katika ile broshua yenye kurasa 32 How Can Blood Save Your Life?
Ikiwa ungependa kupokea nakala, tafadhali jaza na upeleke kuponi inayoandama.
Mimi ningependa kupokea ile broshua yenye kurasa 32 How Can Blood Save Your Life?