Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w91 9/1 uku. 32
  • Imani Yao Katika Mageuzi Ilidhoofishwa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Imani Yao Katika Mageuzi Ilidhoofishwa
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
w91 9/1 uku. 32

Imani Yao Katika Mageuzi Ilidhoofishwa

Mwanamume kutoka Milwaukee, Wisconsin, U.S.A., aliandika mwaka jana kuonyesha uthamini wake “kwa kile kifaa kizuri ajabu kilichoandaliwa katika kitabu Life—How Did It Get Here? By Evolution or by Creation?” Alieleza hivi:

“Miaka miwili iliyopita, nilikutana na wenzi wa ndoa kutoka Beijing, China, waliokuwa wakienda kwenye chuo cha utabibu huku Milwaukee. Walikuwa wastadi wa bayokemia, nao hawakuficha kwamba walikuwa na imani ya moyo mweupe katika mageuzi.

“Kwa uhakika walinipita kwa maarifa ya kisayansi nisiweze kuongea nao kisayansi, kwa hiyo niliamua kuacha kitabu kifundishe. Tulipoendelea na funzo letu, niliweza kuona uhakika wao katika mageuzi ukianza kuyumbayumba.”

Funzo la kitabu chote lilikamilishwa, na yule mwanamume kutoka Milwaukee amalizia hivi: “Biblia imekuwa kwao chanzo cha kweli cha habari. Asante tena kwa kifaa hicho kizuri ajabu.”

Ikiwa ungependa kupokea kitabu hicho cha kurasa 256 chenye vielezi vyenye kupendeza, tafadhali jaza na kupeleka hati-anwani hii yenye kuandama.

[Picha katika ukurasa wa 32]

Mbuni alihitajiwa kwa ajili ya kigumba hiki

Je! mbuni hakuhitajiwa kwa ajili ya chembe ya DNA? Ningependa kupokea kitabu Life—How Did It Get Here? By Evolution or by Creation?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki