Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w91 10/1 uku. 32
  • Amkeni Yasaidia Kushinda Zawadi Italia!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Amkeni Yasaidia Kushinda Zawadi Italia!
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
w91 10/1 uku. 32

Amkeni Yasaidia Kushinda Zawadi Italia!

Mwaka jana msichana wa shule mwenye umri wa miaka kumi katika Italia aliandika insha yenye kichwa “Ikiwa Dunia Ingeweza Kuongea.” Kichwa hicho kilikuzwa kikiwa maongezi kati ya dunia na kitoto aliyekuwa ameiuliza dunia kwa nini ilikuwa inalia. Msichana huyo wa shule aliendelea kusema hivi:

“Dunia ilijibu kwamba ilikuwa imechafuliwa na mchanganyiko wa moshi na ukungu uliokuwa umesababisha hali ya hewa yenye joto jingi. Dunia ikaendelea kuongea na kitoto na kusema kwamba, karibuni mambo yangebadilika na wakati ujao wayo ungekuwa afadhali yajapokuwa yale anayotenda mwanadamu. Tumaini la dunia lilikuwa katika Mungu Mweza Yote, Muumba wayo, ambaye hakuiumba dunia ukiwa bali ili ikaliwe na watu.—Isaya 45:18.”

Msichana huyo wa shule akaeleza hivi: “Nilipata habari hiyo katika magazeti ya Amkeni! (katika Kiingereza) ya Julai 22, 1989; Septemba 8, 1989; na Septemba 22, 1989. Kwa sababu ya magazeti hayo, insha yangu ilishinda zawadi ya kwanza. Na zawadi ya pili ikashindwa na mmoja wa wanafunzi wenzangu ambaye mama yake ni mmoja kati ya wale ambao hupelekewa magazeti kwa kawaida na mama yangu. Yeye pia alipata habari katika magazeti hayo hayo ya Amkeni!

“Ninawashukuru kwa habari hiyo iliyo nzuri na sahihi na rahisi pia inayotufanya tuwe wenye hekima. Zawadi niliyoshinda ni kiasi cha lira 100,000 [karibu dola 100, ya U.S], nami napeleka pesa hizo ili zitumiwe kuchapa magazeti zaidi.”

Tunaona kwamba hata uwe katika dini ipi, wewe pia utanufaishwa na makala zenye kuvutia katika Amkeni!

Ningependa kupelekewa gazeti Amkeni! kwa njia ya posta.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki