Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w92 4/15 uku. 32
  • Wagibeoni- Walitafuta Amani

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wagibeoni- Walitafuta Amani
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
w92 4/15 uku. 32

Wagibeoni- Walitafuta Amani

Mji ulioko kwenye kilima hapo juu unatambulishwa kuwa kwenye mahali ambapo Gibeoni wa zamani ulipokuwa, kilometa 10 hivi kaskazini mwa Yerusalemu.

Yaelekea unajua kwamba Gibeoni ulipata umashuhuri punde baada ya Yoshua kuongoza Israeli katika Bara Lililoahidiwa na kuushinda Yeriko. Wakanaani wa Gibeoni walitambua kwamba wasingeweza kushinda Israeli, ambalo kwa kweli lilikuwa na utegemezo wa kimungu. Ni jambo gani lipasalo kufanywa? Wakiamua kutumia werevu, Wagibeoni walituma wajumbe waliojifanya kuwa wasafiri wa kutoka bara la mbali. Jitihada hiyo ya kupata amani ilifanikiwa, kwani Israeli lilifanya agano pamoja nao. Hila yao ilipofunuliwa, Wagibeoni wakawa wakusanyaji kuni na wachotaji maji.

Kwa wazi Mungu hakuchukizwa na watu hao waliotafuta amani. Alitegemeza vita ya Yoshua ya kuwalinda Wagibeoni waliposhambuliwa na wafalme watano. Yehova hata alifanya ule muujiza wa kuurefusha mchana kwa sababu ya pigano hilo.—Yoshua 9:3-27; 10:1-14.

Wachimbaji walipata kwenye kilima hicho shimo au ziwa lenye kina lililochimbwa katika mwamba. Wagibeoni waliweza kuteremka ngazi kuingia humo na kupata maji kutoka kwa chumba cha chini. Je! hilo lingeweza kuwa lile “ziwa la Gibeoni” lililotajwa kwenye 2 Samweli 2:13? Waakiolojia walivumbua pia vyumba vya chini vilivyochimbwa katika mwamba na vifaa vingine vingi sana vya kutengenezea divai. Naam, yaonekana kwamba Gibeoni ulikuwa kitovu cha kutengenezea divai.

Katika wakati wa Daudi lile hema, au tabenakulo, ya Mungu wa kweli ilikuwa hapo. Mfalme Sulemani alikuja hapa kutoa dhabihu. Yehova alijitokeza kwa Sulemani katika ndoto na kumwahidi “moyo wa hekima na wa akili,” pamoja na mali. (1 Wafalme 3:4-14; 2 Mambo ya Nyakati 1:3) Makala iliyoko kwenye kurasa 12-17 ya toleo hili inaonyesha kwamba wazao wa watu wale walioishi hapa Gibeoni walipendelewa kipekee miongoni mwa taifa la Mungu katika wakati wa baadaye. Je! wewe wajua ni kwa jinsi gani?

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 32]

Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki