Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w92 9/1 uku. 32
  • Mavuno ya Mweneza Evanjeli wa Kweli

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mavuno ya Mweneza Evanjeli wa Kweli
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
w92 9/1 uku. 32

Mavuno ya Mweneza Evanjeli wa Kweli

WILLIAM R. BROWN alienda Afrika kwa mara ya kwanza katika 1923. Akiwa na mke na mtoto wake, ‘alifanya kazi ya mweneza evanjeli’ katika Gambia, Ghana, Liberia, Nigeria, na Sierra Leone. (2 Timotheo 4:5, NW) Mazao ya kazi yake yanashangaza.

Mzawa huyo wa West Indies hakuwa mshiriki wa mojawapo ya makanisa ya Jumuiya ya Wakristo na kwa hakika hakuhusika katika siasa. Badala ya hivyo, alimwiga Yesu na mitume kwa kujulisha wazi jina na enzi kuu ya Yehova, akikazia umaana wa fidia, na kuhubiri habari njema ya Ufalme. (Mathayo 9:35; 20:28; Yohana 17:4-6) William R. Brown alitumia Biblia daima, akiielekezea kuwa ndiyo mamlaka ya mwisho katika mambo ya mafundisho na imani. (2 Timotheo 3:16) Alisisitiza sana juu ya jambo hilo hivi kwamba alijulikana kuwa Bible Brown.

Kwa baraka ya Yehova, mbegu zilizopandwa na Bible Brown zilimea na kukua. Leo, katika nchi alimoongoza njia, Waafrika karibu 200,000 wameweka maisha zao wakfu kwa Muumba wao, nao pia, huhubiri habari njema za Ufalme kwa wengine. (Mathayo 24:14; 1 Wakorintho 3:6-9) Wakristo hao wenye bidii hujulikana kote kwa ajili ya unyoofu na kutegemeka kwao. Wanaonea fahari kuwa Mashahidi wa Yehova na raia wa Kristo, Mfalme anayetawala.

Mavuno ya jinsi hiyo ni matokeo ya uenezaji evanjeli wa Kikristo wa kweli. Mavuno kama hayo yanapatikana kotekote ulimwenguni kwenye bara lolote linalokaliwa na watu. Katika nchi zaidi ya 200, wanaume na wanawake wenye mioyo misikivu zaidi ya milioni nne “wamevunwa” nao wanarudia kuwaambia wengine maneno yaleyale ya yule malaika mweneza evanjeli: “Mcheni Mungu, na kumtukuza kwa maana saa ya hukumu yake imekuja.” (Ufunuo 14:7) Kwa kweli, njia ya pekee ya kupata tumaini katika enzi yetu yenye matatizo ni kumgeukia Mungu na kujitiisha kwa utawala wake wa Ufalme.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki