Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w92 10/1 uku. 32
  • ‘Mbingu Zatangaza . . . ’

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • ‘Mbingu Zatangaza . . . ’
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
w92 10/1 uku. 32

‘Mbingu Zatangaza . . . ’

Karibu kilometa milioni 150 kutoka mahali ulipo sasa, jua hung’aa kwa uangavu mwingi sana angani. Ingawa limeabudiwa kwa maelfu ya miaka likiwa kijimungu, kinyume cha hilo, jirani wetu mtukufu wa kimbingu, ni ushuhuda wa uwezo wa Muumba walo, “aliyezifanya mbingu na nchi.” (Zaburi 115:15) Uangavu na ujoto walo ni wa muhimu kwa uhai duniani. Na mambo ya hakika ambayo wanasayansi wamejifunza juu yalo yanatushangaza sana.

Tunaambiwa kwamba jua hutokeza nishati nyingi sana ajabu. Je! wajua ya kwamba dunia hutumia punde ya kiasi cha nusu moja kati ya bilioni cha joto na nuru ambayo jua hutoa? Hata hivyo kiasi hicho hujumuika kila dakika kuwa nguvufarasi bilioni 240!

Jua hufanyizaje nishati hiyo yote? Ni kwa kutumia tanuri kubwa mno la nyukilia lililomo katika kiini chalo ambalo hutokeza nishati kwa kutwaa tani milioni 3.6 za haidrojeni kila sekunde. Kwa furaha ya ainabinadamu, kuna viwashio vya kutosha katika jua vya kuendeleza taratibu hiyo kwa mabilioni ya miaka.

Mambo mengine ambayo wanasayansi wamevumbua hutokeza maswali ya ziada. Kwa mfano, jua hutikisika daima, kama bamba la chuma ambalo limepigwa kwa nyundo. Kwa nini? Pia, fikiria hili: Kiini cha jua kinachowaka ndiyo sehemu yalo yenye joto jingi zaidi na kadiri tabaka lilivyo mbali kutoka kiini, ndivyo lilivyo lenye ubaridi zaidi. Lakini tunapofikia tabaka la nje ya angahewa ya jua, liitwalo korona, hali yabadilika. Korona ni lenye joto jingi zaidi kuliko yale matabaka yaliyoko karibu zaidi na kile kiini kinachowaka. Kwa nini?

Zaidi ya hayo, ingawa—kama vile dunia—jua huzunguka, sehemu tofauti huzunguka zikiwa na kasi tofauti. Kwa mfano, sehemu ya juu huzunguka kwa kasi zaidi ya matabaka yaliyomo ndani. Kwa nini? Na hilo huwezekanaje? Halafu kuna madoa ya jua. Madoa hayo hutokea na kutoweka kwa kawaida katika kipindi cha miaka 11. Kwa nini hayo hubadilika kwa kawaida jinsi hiyo?

Ingawa kuna mambo mengi zaidi ya kujifunza juu ya jua, yale tunayojua tayari yanatufanya tuwe na kicho kingi cha Muumba walo, Yehova. Kila wakati tunapoliona jua, tunakumbushwa kwamba “mbingu zauhubiri [zautangaza, NW] utukufu wa Mungu, na anga laitangaza kazi ya mikono yake.”—Zaburi 19:1.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki