Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w92 10/15 uku. 32
  • Unabii Watimizwa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Unabii Watimizwa
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
w92 10/15 uku. 32

Unabii Watimizwa

WAKATI Kristo Yesu alipoombwa na wanafunzi wake ishara ya kuwapo kwake kusikoonekana katika mamlaka ya Ufalme, Yesu alitabiri “ongezeko la uhalifu.” (Mathayo 24:3, 12, HNWW) Je! unabii huo unatimizwa katika siku yetu?

Kwa kweli unatimizwa! Kitabu The United Nations and Crime Prevention, kilichotangazwa kwa chapa na UM katika Oktoba 1991, hutaarifu hivi: “Uhalifu mbaya ni tatizo kubwa hasa kwa mataifa mengi ya ulimwengu. Uhalifu wa nchini umezidi kabisa udhibiti wa mataifa mengi moja moja na uhalifu wa kimataifa umeongezeka kwa kasi zaidi kupita uwezo wa sasa wa jumuiya ya kimataifa. . . . Uhalifu unaofanywa na vikundi vilivyopangwa vya wahalifu umepanuka kufikia viwango vya kutisha, kukiwa na matokeo mabaya hasa kwa habari ya jeuri ya kimwili, matisho na ufisadi wa maofisa wa shughuli za umma. Uharamia umesababisha vifo vya makumi ya maelfu ya watu wasio na hatia. Uuzaji dawa za kulevya ili kujifaidi umekuwa msiba wa ulimwenguni pote. Uharibifu wa kimazingira unaofanywa kihalifu bila kujali umekuwa wa namna nyingi wenye kiasi cha kutisha hivi kwamba umekuja kutambuliwa kuwa uhalifu dhidi ya ulimwengu wenyewe.”

Mashambulio: Ongezeko kutoka mashambulio 150 kwa kila watu 100,000 katika 1970 hadi karibu 400 kwa kila 100,000 katika 1990.

Wizi: Ongezeko kutoka zaidi kidogo ya 1,000 kwa kila 100,000 katika 1970 hadi 3,500 kwa kila 100,000 katika 1990.

Mauaji ya kimakusudi: Katika nchi zinazositawi, ongezeko kutoka 1 hadi 2.5 kwa kila 100,000 kati ya 1975 na 1985. Katika nchi zilizositawi ongezeko katika kipindi icho hicho kilikuwa kutoka chini ya 3 hadi zaidi ya 3.5.

Uhalifu unaohusiana na dawa za kulevya: Kitabu hicho huonelea hivi: “Miunganisho mikubwa ya uuzaji [dawa za kulevya] yaweza kuwa na matumizi mengi mno na bunduki nyingi mno kushinda Serikali za mataifa madogo, na kufikia sasa imeweza kuzuia jitihada za kupiga marufuku na za kutekeleza sheria za nchi zilizositawi kiviwanda.”

Kiwango cha ujumla cha uhalifu: Kilitazamiwa kuongezeka maradufu kutoka 4,000 kwa kila 100,000 katika 1985 hadi kufikia karibu na 8,000 mwaka wa 2000.

Ongezeko la uhalifu duniani pote ni sehemu moja tu ya unabii wa Yesu unaoonyesha kwamba tunaishi katika “umalizio wa mfumo wa mambo.” (Mathayo 24:3, NW) Yesu alisema hivi: “Nanyi kadhalika mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu.”—Luka 21:31.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki