Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w92 11/1 uku. 32
  • Alijishindia Zawadi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Alijishindia Zawadi
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
w92 11/1 uku. 32

Alijishindia Zawadi

“NAWIWA na nyinyi,” aandika Kioye, mwanafunzi wa darasa za juu katika shule ya upili, kwa ofisi la tawi la Watch Tower Society katika Japani. Anashukuru sana hivyo kwa ajili ya nini? Kioye alijishindia hivi karibuni zawadi ya juu zaidi katika shindano la insha la kitaifa, lililodhaminiwa na Shirika la Japani la Usalama wa Kuendesha Magari. Tuzo hilo lenye thamani latia ndani safari ya kwenda Uswedi.

Kioye aliandika kuonyesha uthamini wake kwa ajili ya vichapo vizuri vingi vinavyotangazwa na Watch Tower Bible and Tract Society, ambavyo yeye ahisi ndivyo vilivyomsaidia sana afaulu. Kando ya shindano hilo, yeye amewakilisha shule yake katika mashindano mengi ya usemi na insha. “Katika mengi ya mashindano hayo,” yeye asema, “kichwa kinatolewa, na wanafunzi wanafanya utafiti kwa ajili ya insha zao katika maktaba. Hata hivyo, mimi sihitaji kujitaabisha sana jinsi hiyo. Mimi hupata habari nzuri ajabu kwenye rafu ya vitabu nyumbani!” Yeye aendelea: “Kichwa kiwe ni nini, kiwe ni matatizo ya kuzeeka, mazingira, mahusiano ya kimataifa, au kujifanyia maendeleo ya kibinafsi, kwa kawaida kuna mazungumzo yenye kina katika magazeti ya Mnara wa Mlinzi au Amkeni!”

Hata hivyo, si vichapo tu vilivyomsaidia Kioye. Yeye asema kwamba elimu aliyopokea kupitia programu za mafundisho za Mashahidi wa Yehova ilimsaidia afanyie maendeleo kusoma na kuandika kwake, na hilo lilimwezesha afane zaidi katika mashindano hayo. “Wakati mmoja, nilitaka sana kupata elimu ya chuo kikuu,” yeye akiri. “Lakini ningeweza kupata wapi mazoezi kama haya?” Sasa anatumaini kufanya kazi wakati wote katika kuwasaidia wengine wanufaike kutokana na elimu ambayo amepokea. Ingawa amefurahia zawadi hiyo ya insha, moyo wa Kioye umekazwa juu ya kujishindia zawadi ya uhai.—Linganisha Wafilipi 3:14.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki