Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w93 5/15 uku. 30
  • Epuka Roho ya Kiburi!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Epuka Roho ya Kiburi!
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
w93 5/15 uku. 30

Epuka Roho ya Kiburi!

Mithali ya Biblia yenye hekima husema hivi: “Auinuaye sana mlango wake hutafuta uharibifu.” (Mithali 17:19) Kuna ubaya gani na mlango ulioinuliwa sana? Na ni nini jambo kuu la mithali hiyo?

KATIKA nyakati za kale watu mmoja mmoja na vikundi vya wanyang’anyi waliopanda farasi walikuwa wa kawaida. Nyumba zisizokuwa na ulinzi katika eneo la wazi zilikuwa rahisi kushambuliwa na wezi. Ili kuzuia mali zao zisiporwe, baadhi ya wenye nyumba walijenga ukuta wenye lango la pekee. Ukuta ulikuwa mrefu, lakini lango lilikuwa la chini. Kwa kweli, mengine hayakuzidi urefu wa meta moja—chini mno yasiweze kuingiwa na farasi pamoja na mpanda farasi wake. Wale ambao hawakufanya mlango wao kuwa wa chini walikuwa na hatari ya kuingiliwa na wapanda farasi na kuporwa mali zao.

Katika majiji kwa kawaida milango ya ua ilikuwa ya chini na hayakuvutia, ili isitoe ishara yoyote ya utajiri ambao huenda ukawa ulikuwamo ndani ya makao hayo yaliyozingirwa. Hata hivyo, katika Uajemi lango lenye fahari lilikuwa mojawapo ishara za kifalme, ambazo baadhi ya raia walijaribu kuiga kwa hatari kubwa. Yeyote aliyetengenezea nyumba yake lango lililoinuliwa (ya hali ya juu) sana alikuwa akialika unyang’anyi kwa sababu ya wonyesho wake wa ufanisi.

Hivyo Mithali 17:19 huonyesha kwamba wale walioinua sana mlango wao walikuwa wakialika msiba kwa kujionyesha wenyewe kuwa wenye thamani nyingi zaidi ya vile walivyokuwa. Mithali hiyo yaweza pia kurejezea kinywa kikiwa mlango ulioinuliwa sana kwa usemi wenye majivuno na wenye kiburi. Maongeo hayo huchochea ugomvi na yaweza hatimaye kumwongoza mtu huyo mwenye majivuno kwenye msiba. Kwa hiyo, ni jambo la hekima kama nini kuepuka roho ya kiburi!

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 30]

Picturesque Palestine, Sinai and Egypt, Buku 1, ya Colonel Wilson (1881)

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki