Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w93 10/1 uku. 32
  • Je! Umepata Kuanzisha Moto wa Msitu?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Umepata Kuanzisha Moto wa Msitu?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
w93 10/1 uku. 32

Je! Umepata Kuanzisha Moto wa Msitu?

BILA SHAKA LA, wewe wasema. Lakini ebu ngoja! Labda umepata kufanya hivyo. Sikiliza maneno ya mwanafunzi Yakobo: “Ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.”—Yakobo 3:5.

Ulimi ni kiungo muhimu cha usemi, lakini umetumiwa vibaya kama nini! Watu hutumia ulimi kusema uwongo na kuchongea. Wao huutumia kuchambua wengine vikali, kuharibu sifa zao, na kuwapunja. Wachochea-ghasia hutumia ulimi kuanzisha mapinduzi. Adolf Hitler alitumia ulimi wake kukusanya taifa kwa ajili ya vita—‘moto wa msitu’ kwelikweli!

Hata wale wenye nia njema wanaweza kusababisha ‘mioto midogo ya msitu.’ Je! umepata kusema jambo fulani kisha mara iyo hiyo ukajuta kwa nini ulilisema? Ikiwa ndivyo, waelewa kile ambacho Yakobo alimaanisha aliposema: “Ulimi hakuna awezaye kuufuga.”—Yakobo 3:8.

Hata hivyo, tunaweza kujaribu kuutumia ulimi wetu vema. Kama vile mtunga-zaburi, twaweza kusema hivi kwa kuazimia: “Nitazitunza njia zangu nisije nikakosa kwa ulimi wangu.” (Zaburi 39:1) Badala ya kuwachambua wengine vikali, tunaweza kujaribu kuwajenga. Badala ya kuchongea watu, tunaweza kusema mema juu yao. Badala ya kupunja na kudanganya, tunaweza kusema kweli na kufundisha. Unapochochewa na moyo mwema, ulimi unaweza kusema maneno ya ajabu ya kuponya. Yesu alitumia ulimi wake katika njia nzuri ajabu kuifundisha ainabinadamu juu ya wokovu.

Kwa kweli, “mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi.” (Mithali 18:21) Je! ulimi wako ni wenye kudhuru au wenye kutoa uhai? Je! unaanzisha ‘mioto ya msitu’ au kuizima? Mtunga-zaburi alisali hivi kwa Mungu: “Ulimi wangu na uiimbe ahadi yako, maana maagizo yako yote ni ya haki.” (Zaburi 119:172) Tukisitawisha mtazamo wa mtunga-zaburi, sisi pia tutautumia ulimi wetu vema.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 32]

Picha ya U.S. Forest Service

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki