Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w93 11/15 uku. 32
  • Kama Mti

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kama Mti
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
w93 11/15 uku. 32

Kama Mti

“MASHAIRI hubuniwa na wapumbavu kama mimi, lakini ni Mungu tu awezaye kuubuni mti.” Kwa njia ya kuadhimisha mema mengi ya miti, mtunga-mashairi Joyce Kilmer alimpa Mungu sifa ya kuumbwa kwayo.

Yehova Mungu amefanya miti ya unamna-namna mwingi, fahari nyingi, na matumizi mengi. Miti midogo sana, na pia miti mikubwa mno, yaweza kuwa mizuri sana hivi kwamba haisimuliki. Zaidi ya hayo, miti huandaa chakula, dutu (viwashio), na makao. Na wabuni huendelea kupata matumizi mapya ya mbao.

Katika Biblia, nyakati nyingine miti hutumiwa kwa ufananisho kuwakilisha falme, watawala, na watu mmoja-mmoja. (Ezekieli 31:1-18; Danieli 4:10-26) Miti inatajwa kuhusiana na hali zenye shangwe, amani, na mazao yaliyotokana na ufalme wa Yehova na kurejeshwa kwa watu wake. (1 Mambo ya Nyakati 16:33; Isaya 55:12; Ezekieli 34:27; 36:30) Maandiko huahidi pia kwamba siku za watu wa Mungu zitakuwa kama zile za mti. (Isaya 65:22) Hilo lina maana sana tung’amuapo kwamba miti mingine huishi kwa muda wa karne nyingi.

Mtunga-zaburi wa Kibiblia alisema kwamba mtu apendezwaye na sheria ya Mungu “atakuwa kama mti uliopandwa kandokando ya vijito vya maji, uzaao matunda yake kwa majira yake, wala jani lake halinyauki; na kila alitendalo litafanikiwa.” Mti wenye kusitawi uliopandwa karibu na chanzo chenye maji mengi ulimkumbusha mtunga-zaburi juu ya ufanisi wa kiroho unaofurahiwa na mtu ambaye “sheria ya BWANA [Yehova, NW] ndiyo impendezayo.” (Zaburi 1:1-3) Ukipendezwa kikweli na sheria na Neno Takatifu la Mungu, siku zako zaweza kuwa kama zile za mti. Kwa kweli, kwa kutenda kulingana na ujuzi sahihi juu ya Yehova Mungu na Yesu Kristo, waweza kuwa na tumaini la uhai wa milele.—Yohana 17:3.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki