Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w94 1/15 uku. 32
  • Kama Matofaa ya Dhahabu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kama Matofaa ya Dhahabu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
w94 1/15 uku. 32

Kama Matofaa ya Dhahabu

MATOFAA—jinsi yapendezavyo jicho na kinywa pia! Biblia hutumia tunda hilo tamu sana katika tashbiha (usemi ambao hulinganisha vitu) yenye kuchochea fikira isemapo hivi: “Neno linenwalo wakati wa kufaa. Ni kama machungwa [matofaa ya dhahabu, NW] katika vyano vya fedha.” (Mithali 25:11) Ni nini kinachomaanishwa na taarifa hiyo?

“[Matofaa ya dhahabu, NW] katika vyano vya fedha” huenda ikaonyesha kitu kilichochongwa, kama vile sinia ya fedha iliyochongwa yenye matunda ya dhahabu juu yayo. Kwa kuwa mistari ya mapema katika sura hiyo hutaja juu ya kumwendea mfalme, mstari huo ungeweza kurejezea zawadi zilizopewa mtawala—mapambo ya dhahabu yenye maumbo ya matofaa yaliyowekwa juu ya sinia za fedha. (Mithali 25:6, 7) Ni yenye uzuri wa kuvutia, kwelikweli!

Kuna uzuri uo huo katika maneno yafaayo, yenye adhama, ya wakati ufaao, yawe yameandikwa au kusemwa. Hayo hupendeza, hutia moyo, nayo hunufaisha katika njia nyingi. Hasa maneno yaliyo ndani ya Biblia ambayo yamepuliziwa kimungu ni kama “matofaa ya dhahabu [yenye uzuri] katika vyano vya fedha.”

Kama ionyeshwavyo na maneno yenye hekima ya Mfalme Sulemani kwenye Mithali 25:11, yeye “a[li]tafuta-tafuta ili apate kuona maneno yapendezayo, na yale yaliyoandikwa kwa unyofu, yaani, maneno ya kweli.” (Mhubiri 12:10; Mithali 25:1) Karne kadhaa baadaye, mtume Mkristo Paulo aliandika hivi: “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa.” (2 Timotheo 3:16) Ndiyo, Biblia ina shauri, unabii, vifananishi, na kweli zifaazo zenye mng’ao na uzuri mwingi hivi kwamba zapita sana kazi za wasanii walio stadi zaidi. Zaidi ya hayo, yeyote apataye hekima kutoka katika Neno la Mungu, Biblia, hupata mali yenye thamani kubwa na aweza kuwa na tumaini la uhai wa milele.—Mithali 4:7-9; Yohana 17:3.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki