Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w94 4/15 uku. 32
  • Yenye Thamani Kuliko Marijani

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yenye Thamani Kuliko Marijani
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
w94 4/15 uku. 32

Yenye Thamani Kuliko Marijani

Idadi zenye kuongezeka za watalii zimesisimuka juu ya maonyesho kama hili lililo katika maji ya Bahari Nyekundu.

Wale samaki wasiohesabika wa rangi nyingi mbalimbali wanasisimua kwa wale wanaoogelea katika maji hayo maangavu. Lakini angalia kwamba kotekote kando ya samaki hao wenye rangirangi wanaoonekana hapa, kuna wonyesho wenye kuvutia macho wa maajabu mengine ya baharini kutia na marijani zenye rangi nyangavu.

Marijani hizo zenye kupendeza zaweza kupatikana katika miundo na rangi nyingi. Kama uwezavyo kuwazia, hata katika nyakati za kale vipande vya marijani vyenye urembo vilithaminiwa sana. Wasanii walivitumia kufanyiza mapambo mazuri, na waandishi wa Biblia walitaja marijani pamoja na dhahabu, fedha, na akiki. (Mithali 3:14, 15; Ezekieli 27:16) Lakini waandishi hao watusaidia tuone zaidi ya uzuri na thamani ya marijani zenyewe.

Walikazia kwamba mambo fulani ni yenye thamani hata zaidi na kwamba twapaswa kuyathamini sana. Mke mwema, mwenye uwezo ni mmoja wayo, kwani twasoma hivi: “Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.” (Mithali 31:10) Je! wewe ni mwanamume aliyeoa? Tazama tena kwenye marijani hizi nzuri sana, na uone kama unamstahi mke wako kama astahilivyo.

Iwe sisi ni wanaume au wanawake, waliofunga ndoa au waseja, kuona marijani zenye uzuri sana kwapaswa kutusaidie tuthamini ile thamani iliyo kuu hata zaidi, ya hekima, ya ufahamu, na ya ujuzi wa kimungu. Neno la Mungu husema hivi: “Heri [mwenye furaha ni, NW] mtu yule aonaye hekima, na mtu yule apataye ufahamu. Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi. Yeye ana thamani kuliko marijani, wala vyote uvitamanivyo havilingani naye.”—Mithali 3:13-15; 8:11.

Kwa hiyo iwe twayaona wenyewe kwa kuogelea au kupitia picha, marijiani za Bahari Nyekundu zapaswa zituwasilishie uzuri na pia habari ya kufikiriwa kwa njia yenye mafaa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki