Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w94 5/15 uku. 3
  • Je! Unaithamini Biblia?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Unaithamini Biblia?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Habari Zinazolingana
  • “Tazama! Kijakazi wa Yehova!”
    Igeni Imani Yao
  • “Tazama! Kijakazi wa Yehova!”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Mfano wa Maria Unatufundisha Nini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Alikabiliana na Upanga wa Majonzi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2014
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
w94 5/15 uku. 3

Je! Unaithamini Biblia?

MUDA uzidio tu miaka 200 iliyopita, Mary Jones alizaliwa katika Llanfihangel, kijiji cha mashambani cha Wales ambacho hakikuwa mbali na pwani ya Atlantiki. Wazazi wake walikuwa wafumaji maskini—kiasi cha kwamba hawangeweza kuwa na Biblia. Lakini walikazia binti yao upendo kwa Mungu kwa kumsimulia hadithi za Biblia na kurudia maandiko waliyokumbuka. Mara nyingi Mary alikuwa akisoma Biblia ya Kiwales ya jirani naye akaanza kuweka akiba ya fedha kidogo ambazo alikuwa akipata, akiwa ameazimia kununua Biblia yake mwenyewe.

Katika mwaka wa 1800, Mary alipokuwa na miaka 16, alisikia kwamba Biblia chache za Kiwales zilikuwa zikiuzwa umbali wa kilometa 40 katika mji mdogo wa Bala. Kwa ujasiri, aliazimia kwenda huko kwa miguu. Na akafanya hivyo, akivuka milima kwa miguu mitupu. Hata hivyo, alipofika huko, nakala zote zilikuwa zimenunuliwa. Mary akagundua pia kwamba kiasi cha fedha alizoweka akiba kilikuwa kidogo sana.

Pasta wa sehemu hiyo alivutiwa sana na ujuzi na upendo ambao Mary alikuwa nao kwa Biblia. Akiona machozi yake ya kuvunjika moyo baada ya kujitahidi sana, kwa fadhili alimpa nakala yake mwenyewe, akisema hivi: “Uisome kwa makini, ujifunze kwa bidii, uyakariri maneno matakatifu, na uishi kwa kupatana na mafundisho yayo.”

Baadaye kisa hicho kilisimuliwa katika mkutano wa Halmashauri ya Religious Tract Society of London. Katika mkutano huo, uamuzi ulifanywa wa kuandaa tafsiri za Biblia kwa watu wa Wales na vilevile kwa ulimwengu wote. Kuanzia mwanzo huo mdogo kukatokea shirika la kwanza kati ya mashirika mengi ya Biblia ya karne ya 19. Baada ya hapo, nakala za Biblia katika lugha za kigeni zilianza kutokea kwa ukawaida zaidi.

Leo, Watch Tower Bible and Tract Society, lililokuwa shirika rasmi katika 1884, huchapisha Biblia na vichapo vya kusaidia kujifunza Biblia kwa lugha zaidi ya 200. Limegawanya ulimwenguni kote nakala milioni 72 za Biblia ya lugha ya kisasa ya New World Translation of the Holy Scriptures. Likiwa limetafsiriwa kutoka Kiebrania na Kigiriki cha awali, New World Translation sasa yapatikana kwa ukamili au kwa sehemu katika lugha 18 na sasa yaendelea kutafsiriwa katika ndimi nyinginezo 12.

Kwa kuwa sasa karibu kila mtu aweza kupata Biblia, unaionaje? Je! unathamini Biblia? Je! una nakala unayothamini na kusoma?

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 3]

Kutoka kwa kitabu The Story of Mary Jones and Her Bible

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki