Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w94 7/15 uku. 25
  • Sherehe za Siku ya Kuzaliwa Zimetokeza Vifo Vingi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Sherehe za Siku ya Kuzaliwa Zimetokeza Vifo Vingi
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
w94 7/15 uku. 25

Sherehe za Siku ya Kuzaliwa Zimetokeza Vifo Vingi

SHEREHE ya siku za kuzaliwa huonwa na watu wengi kuwa desturi tu isiyodhuru. Lakini Biblia haionyeshi desturi hiyo kuwa nzuri. Isitoshe, Maandiko hayaonyeshi kamwe kwamba watumishi wa Mungu waaminifu walisherehekea siku za kuzaliwa.

Sherehe mbili tu za siku ya kuzaliwa zinazotajwa na Biblia zilifanywa na watawala waliokuwa maadui wa Mungu. Kila sherehe ilihusisha uuaji, ili wageni watazame kwa furaha kifo cha mtu aliyemkasirisha mfalme. Katika kisa cha kwanza, Farao, mfalme wa Misri, aliua mkuu wa waokaji. (Mwanzo 40:2, 3, 20, 22) Mtawala huyo wa Misri alifanya hivyo wakati wa karamu kwa sababu alikuwa amemghadhabikia mtumishi wake. Katika kisa cha pili, Herode, mtawala wa Galilaya aliyekosa adili, alimkata kichwa Yohana Mbatizaji ili ampendeze msichana ambaye alikuwa amemfurahisha kwa jinsi alivyosakata dansi. Hizo ni mandhari za kuchukiza kama nini!—Mathayo 14:6-11.

Lakini, je, Biblia haijaelekeza fikira kwa sherehe za siku ya kuzaliwa zilizopita kiasi sana? La hasha. Mwanahistoria wa kale wa Kiyahudi Yosefo afunua kwamba visa hivyo havikuwa vya kipekee. Yeye aandika juu ya visa vingine vya mauaji yaliyofanywa katika sherehe za siku ya kuzaliwa kwa ajili ya utumbuizo.

Kwa kielelezo, baadhi ya mauaji yalitokea baada ya uharibifu wa Yerusalemu mwaka wa 70 W.K., wakati Wayahudi 1,000,000 walikufa na wengine 97,000 wakaokoka na kuchukuliwa mateka. Wakiwa njiani kuenda Roma, jemedari Tito wa Waroma alipeleka mateka wake Wayahudi kwenye bandari ya Kaisaria iliyokuwa karibu.

Yosefo aandika hivi: “Tito alipobaki Kaisaria, alisherehekea siku ya kuzaliwa ya ndugu yake Domitiani kwa ufahari mwingi mno, akiwaua mateka zaidi ya 2,500 katika michezo iliyohusisha wanyama-mwitu na miale ya moto. Baada ya hapo akaenda Beritus [Beirut], iliyokuwa himaya ya Waroma katika Foenike, ambako alisherehekea siku ya kuzaliwa ya baba yake kwa kuua mateka wengine wengi zaidi katika maonyesho yenye ufahari mwingi sana.”—The Jewish War, 7, 37, iliyotafsiriwa na Paul L. Maier katika Josephus: The Essential Writings.

Haishangazi kwamba kamusi The Imperial Bible-Dictionary yaeleza kwamba: “Waebrania wa baadaye waliziona sherehe za siku ya kuzaliwa kuwa sehemu ya ibada ya sanamu, maoni ambayo yalithibitishwa sana na mambo yale waliyoona katika miadhimisho ya kawaida iliyofanywa katika siku hizo.”

Wakristo waaminifu wa karne ya kwanza hawahisi kushiriki katika desturi inayoonyeshwa katika Biblia kuwa mbaya na ambayo ilisherehekewa kwa njia ya ukatili na Waroma. Leo, Wakristo wenye mioyo minyoofu hung’amua kwamba masimulizi ya Biblia kuhusu siku za kuzaliwa yalikuwa miongoni mwa mambo yaliyoandikwa ili kuwafundisha. (Warumi 15:4) Wao huepuka kusherehekea siku za kuzaliwa kwa sababu miadhimisho kama hiyo humpa mtu mwenyewe umaana usiofaa. Na muhimu zaidi, watumishi wa Yehova hufikiria kwa hekima vile Biblia ionyeshavyo sherehe za siku ya kuzaliwa kuwa zisizofaa.

[Picha katika ukurasa wa 25]

Uwanja wa mchezo kule Kaisaria

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki