Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w94 9/15 uku. 32
  • “Mizizi Isiyoondoleka”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Mizizi Isiyoondoleka”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
w94 9/15 uku. 32

“Mizizi Isiyoondoleka”

MIONGONI mwa vitu vya ulimwengu vikubwa zaidi na vidumuvyo kwa muda mrefu zaidi ni miti ya sekuia ya California. Miti hiyo mirefu ajabu hufikia kimo cha meta 90 ikomaapo nayo yaweza kuishi kwa zaidi ya miaka 3,000.

Ingawa sekuia huonekana kuwa wenye kutisha ajabu, mfumo wayo wa mizizi wavutia kadiri iyo-hiyo. Sekuia ina mizizi mingi itandayo iwezayo kuenea katika eneo la hektari 1.2 au 1.6. Mfumo huo wa mizizi huandaa nguzo iliyo ngumu kabisa wakati wa mafuriko ya maji au pepo za juu. Inawezekana hata kwa sekuia kustahimili tetemeko kubwa la ardhi!

Mfalme Sulemani alichagua mfumo wenye nguvu wa mti kuwa mfano katika mojapo methali zake. “Hakuna mtu yeyote awezaye kujisitawisha kwa uovu,” yeye akasema, “lakini wema wana mizizi isiyoondoleka.” (Mithali 12:3, The New English Bible) Ndiyo, waovu hawatasimama kwa uthabiti daima. Mafanikio yoyote waonekanayo kupata ni ya muda mfupi tu, kwani Yehova aahidi kwamba “kutaraji kwao walio waovu kutapotea.”—Mithali 10:28.

Hilo ni onyo kwa wale wanaodai kuwa Wakristo, kwani Yesu alisema kwamba wengine ambao hawangekuwa na “mizizi” ndani yao wangekwazika. (Mathayo 13:21) Na zaidi, mtume Paulo aliandika juu ya watu ambao ‘wangetupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu bandia.’ (Waefeso 4:14) Jambo hilo laweza kuzuiwaje?

Kama vile mizizi ya sekuia itandayo sana katika udongo wa ardhi wenye rutuba, ndivyo akili zetu na mioyo yetu inavyohitaji kuzingatia sana Neno la Mungu na kutwaa ndani yalo maji yalo yenye kuleta uhai. Jambo hilo litatusaidia kusitawisha imani yenye mizizi iliyo thabiti. Bila shaka tutaona matokeo ya majaribu makali kama dhoruba. Huenda hata tukatetemeka, kama mti, chini ya majaribu. Lakini kama imani yetu ina msingi mzuri, tutathibitika kuwa na “mizizi isiyoondoleka.”—Linganisha Waebrania 6:19.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki