Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w94 11/1 uku. 32
  • Kwa Nini Waovu Husitawi?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kwa Nini Waovu Husitawi?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
w94 11/1 uku. 32

Kwa Nini Waovu Husitawi?

“MBONA waovu wanaishi?” Swali hili liliulizwa zamani sana na Ayubu mwaminifu, nalo limerudiwa-rudiwa mara nyingi tangu siku yake. Huenda limo katika akili ya watu wengi katika eneo la iliyokuwa Yugoslavia (kama mwanamke aonyeshwaye kwenye jalada letu) waombolezao kwa ajili ya wale wanaotaabika katika vita vyenye msiba sana. Kwa nini watu waovu huokoka na hata kusitawi? Kama Ayubu alivyoona, mara nyingi “nyumba zao zi salama pasina hofu, wala fimbo ya Mungu haiwapigi.”—Ayubu 21:7, 9.

Je, hii yamaanisha kwamba hakuna maana ya kutumikia Mungu, kupenda jirani yako na kuepuka kufanya mabaya? Sivyo hata kidogo! Biblia hutupa wazo lifaalo wakati isemapo: “Usijaribu kuwashinda watenda maovu au kuiga wale watendao mabaya. Maana kama nyasi watanyauka upesi, na kupotea kama majani mabichi wakati wa masika. Tumaini katika BWANA na utende mema.”—Zaburi 37:1-3, The New English Bible.

Ndiyo, kusitawi kuonekanao kwa waovu ni kwa muda tu. Kwa kweli, maisha yao ni mafupi sana, bali wale wamtumikiao Mungu wana tumaini tukufu la wakati ujao. Karibuni, ahadi ya Mungu itatimizwa: “[Mungu] atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.” (Ufunuo 21:4) Ni waadilifu tu, wala si waovu, watauona wakati huo. Ni kitia moyo kilichoje cha kumkaribia Mungu na kujifunza kufanya mapenzi yake, hata wale wanaotuzunguka wawe waovu jinsi gani!

Ikiwa ungependa habari zaidi au ungependa kutembelewa na mtu fulani ili aongoze funzo la Biblia nyumbani pamoja na wewe bila malipo, tafadhali andikia I.B.S.A., Box 47788, Nairobi, Kenya, au tumia anwani ifaayo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa 2.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki