Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w94 11/15 uku. 32
  • “Hivyo Ndivyo Wakristo wa Kweli Wanavyopaswa Kujiendesha”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Hivyo Ndivyo Wakristo wa Kweli Wanavyopaswa Kujiendesha”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
w94 11/15 uku. 32

“Hivyo Ndivyo Wakristo wa Kweli Wanavyopaswa Kujiendesha”

KATIKA kitabu chake cha 1990 Arbeit macht tot—Eine Jugend in Auschwitz (Kazi Hukuua—Ujanani Katika Auschwitz), mwokokaji Tibor Wohl wa Auschwitz aandika juu ya mazungumzo aliyopata kusikia kati ya wafungwa wawili. Mmoja, Mwaustria, alidai “kutokuwa mwamini.” Hata hivyo, aliwasifu wafungwa waliovalia umbo la pembe-tatu la zambarau—Wanafunzi wa Biblia, kama Mashahidi wa Yehova walivyojulikana kambini.

“Hawaendi vitani,” Mwaustria huyo akamwambia mwenzake. “Ni afadhali kwao kuuawa kuliko waue mtu mwingine yeyote. Kwa maoni yangu hivyo ndivyo Wakristo wa kweli wanavyopaswa kujiendesha. Lazima nikueleze tukio la kupendeza sana nililokuwa nalo pamoja nao. Tulikuwa pamoja na Wayahudi na Wanafunzi wa Biblia katika jengo moja katika kambi ya Stutthof. Katika siku hizo Wanafunzi wa Biblia walilazimika kufanya kazi ngumu, nje kwenye baridi kali. Hatukuelewa jinsi walivyookoka. Walisema Yehova aliwapa nguvu. Walihitaji mkate sana, maana walikuwa na njaa sana. Lakini walifanya nini? Walikusanya chakula chote walichokuwa nacho, wakachukua nusu yacho na nusu ile nyingine wakawapa ndugu zao, ndugu zao wa kiroho, waliokuja wakiwa na njaa sana kutoka kambi nyinginezo. Na waliwakaribisha na kuwabusu. Kabla hawajala, walisali, na baadaye nyuso zao ziling’aa kwa furaha. Walisema kwamba hakuna yeyote aliyekuwa mwenye njaa tena. Basi, waona, halafu nikafikiri, ‘Hawa ni Wakristo wa kweli.’ Hivyo ndivyo nilikuwa nikifikiri wanapaswa kuwa. Ingalikuwa vizuri kama nini kuwapa marafiki wenye njaa ukaribishaji kama huo hapa Auschwitz!”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki