Jinsi Ambavyo Wengine Hutoa Upaji kwa Ajili ya Kazi ya Kuhubiri Ufalme
◻ MICHANGO KWA KAZI YA ULIMWENGUNI POTE: Wengi huweka kando au hupangia kiasi cha fedha ambazo wao hutia katika masanduku ya michango yaliyo na kibandiko hiki: “Michango kwa Kazi ya Sosaiti ya Ulimwenguni Pote—Mathayo 24:14.” Kila mwezi, makutaniko hupeleka kiasi hicho ama kwenye makao makuu ya ulimwengu katika Brooklyn, New York, ama kwenye ofisi ya tawi iliyo karibu zaidi.
◻ ZAWADI: Upaji wa hiari wa fedha waweza kupelekwa moja kwa moja kwenye Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania, 25 Columbia Heights, Brooklyn, New York 11201-2483, au kwenye ofisi ya tawi ya Sosaiti inayotumikia nchi yako. Vito au mali nyingine zenye thamani zaweza kutolewa pia. Barua fupi yenye kutaarifu kwamba hiyo ni zawadi ya moja kwa moja yapasa iambatane na michango hiyo.
◻ MPANGO WA UPAJI WENYE MASHARTI: Fedha zaweza kupewa kwa Watch Tower Society kuwa amana hadi kifo cha mpaji, kukiwa na uandalizi wa kwamba kukiwa na uhitaji wa kibinafsi, zitarudishwa kwa mpaji.
◻ BIMA: Watch Tower Society yaweza kutajwa kuwa mfaidikaji wa mpango wa bima ya maisha au katika mpango wa kustaafu kazi au malipo ya uzeeni. Sosaiti yapasa kujulishwa juu ya mipango yoyote kama hiyo.
◻ AKIBA ZA BENKI: Akiba za benki, hati za amana, au akiba za fedha za kustaafu za mtu mmoja-mmoja zaweza kuwekwa zikiwa amana kwa ajili ya au kuweza kulipwa wakati wa kifo kwa Watch Tower Society, kulingana na matakwa ya benki ya hapo. Sosaiti yapasa kujulishwa juu ya mipango yoyote kama hiyo.
◻ HISA NA DHAMANA: Hisa na dhamana zaweza kupewa Watch Tower Society ama zikiwa zawadi ya moja kwa moja ama zikiwa chini ya mpango ambao mapato yaendelea kulipwa kwa mpaji.
◻ MASHAMBA NA NYUMBA: Mashamba na nyumba ziwezazo kuuzwa zaweza kupewa kwa Watch Tower Society ama kwa kutoa zawadi ya moja kwa moja ama kwa kuweka shamba au nyumba ya maisha kwa ajili ya mpaji, ambaye aweza kuendelea kuishi humo muda wa maisha yake. Mtu apaswa kuarifu Sosaiti kabla ya kuipa Sosaiti hati yoyote ya mashamba na nyumba.
◻ WASIA NA AMANA: Mali au fedha zaweza kupangiwa kuwa urithi wa Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania kwa njia ya wasia wenye kutekelezwa kisheria, au Sosaiti yaweza kutajwa kuwa mfaidikaji wa mkataba wa amana. Amana inayofaidi tengenezo la kidini yaweza kuandaa faida fulani za kodi. Nakala ya wasia au mkataba wa amana yapasa kupelekwa kwa Sosaiti.
◻ UTOAJI ULIOFANYIWA MPANGO: Sosaiti imekusanya habari juu ya “Utoaji Uliofanyiwa Mpango.” Wale wanaopanga kuipa Sosaiti zawadi ya kipekee sasa au kuacha wasia wafapo waweza kupata habari hii kuwa yenye maana. Hiyo ni kweli hasa wakati wanapotaka kutimiza mradi fulani au mpango fulani wa familia wa kupata mali huku wakitumia mapunguzo ya kodi ili kupunguza gharama ya zawadi hiyo au wasia. Habari hii yaweza kupatikana kwa kuandikia Sosaiti kwa kutumia anwani ionyeshwayo hapa chini.
Kwa habari zaidi kuhusu mambo kama hayo, andikia International Bible Students Association, P. O. Box 47788, Nairobi, Kenya.