Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w95 4/15 uku. 32
  • New World Translation Yamvutia Msomi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • New World Translation Yamvutia Msomi
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
w95 4/15 uku. 32

New World Translation Yamvutia Msomi

KULINGANA na msomi wa Kigiriki cha kale Dakt. Rijkel ten Kate, tafsiri ya Biblia ya Kiholanzi haikufasiri maneno fulani kwa njia sahihi. Kwa mfano, katika Luka sura ya 2, tunapata maneno matatu tofauti ya Kigiriki (breʹphos, pai·diʹon, na pais) yaliyotumiwa kufafanua hatua zilizofuatana za ukuzi wa Yesu. Kila moja ya maneno haya yana utofauti kidogo. Hata hivyo, katika Biblia nyingi, maneno haya mawili au yote matatu yamefasiriwa kijuu-juu kuwa “mtoto.” Ni ipi iliyo tafsiri sahihi?

Dakt. ten Kate aeleza kwamba katika mstari wa 12 neno la Kigiriki breʹphos humaanisha “kitoto kilichozaliwa, au kitoto.” Neno Pai·diʹon, lililotumiwa katika mstari wa 27, humaanisha “mvulana mchanga au mtoto,” nalo pais, lipatikanalo katika mstari wa 43, lapaswa kutafsiriwa “mvulana.” “Kulingana na nijuavyo,” Dakt. ten Kate aliandika katika toleo la Machi 1993 la Bijbel en Wetenschap (Biblia na Sayansi), “hakuna tafsiri moja ya Kiholanzi iliyotafsiri maneno haya kwa usahihi, yaani, kwa upatani kabisa na maandiko ya kwanza.”

Baadaye, Dakt. ten Kate alionyeshwa New World Translation of the Holy Scriptures, inayopatikana katika lugha 12, kutia ndani Kiholanzi. Aliitikiaje? “Nimeshangaa sana,” akasema, “kwamba kwa kweli kuna Biblia moja ya Kiholanzi ambamo matumizi tofauti ya maneno ya Kigiriki breʹphos, pai·diʹon, na pais yametafsiriwa ifaavyo.” Je, New World Translation inatafsiri mistari hii kwa kupatana na maandiko ya Kigiriki cha awali? “Inapatana kabisa” ajibu Dakt. ten Kate.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki