Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w95 5/15 uku. 32
  • Sarafu Zenye Jina la Mungu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Sarafu Zenye Jina la Mungu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
w95 5/15 uku. 32

Sarafu Zenye Jina la Mungu

TAZAMA kwa makini kwenye sarafu za fedha zinazoonyeshwa hapa. Zilifanyizwa na mfalme Wilhelm 5 wa Ujerumani wakati wa utawala wake kuanzia 1627 hadi 1637. Wakati huo, Ulaya ya kati ilikuwa katika Vita ya Miaka Thelathini, mzozo kati ya Wakatoliki na Waprotestanti. Wilhelm 5 aliunga mkono kikosi cha Kiprotestanti. Ili kugharimia gharama kubwa ya pigano hilo, alichukua fedha zake zote na kufanyiza sarafu kutokana nazo.

Kwa upendezi, ile michoro kwenye nyingi za sarafu huonyesha jua linalozingira jina la Mungu, Yehova, likiwa kwa namna ya Tetragramatoni za Kiebrania. Pia kuna mti wa mvumo, unaofananisha uwezo. Maana yake ni kwamba mti huo, ujapoinamishwa na upepo, unabaki bila kuvunjika chini ya ulinzi wa Mungu. Mwandiko wa Kilatini kwenye sarafu hiyo una jina Yehova nao waonyesha uhakika wa utunzi wake.

Badala ya kuomba ulinzi wa Mungu, utumizi kama huo wa jina la Mungu kwa kweli ulikuwa bure, kwa kuwa Yehova hajiungi na upande wowote katika mizozo ya kijeuri ya binadamu. Kwa kweli, hiyo Vita ya Miaka Thelathini haingeweza kupokea kibali cha Mungu. “Kulingana na makadirio,” chasema Funk & Wagnalls New Encyclopedia, “zaidi ya nusu ya watu wa Ujerumani walikufa katika vita hiyo. Majiji, miji, vijiji, na mashamba mengi yasiyohesabika ya Ujerumani yaliharibiwa kabisa. Karibu theluthi mbili za majengo ya viwanda, ukulima, na biashara ya Ujerumani yaliharibiwa.”

Utumizi wa jina Yehova kwenye sarafu hizi hutukumbusha ile amri iliyopewa Waisraeli: “Usilitaje bure jina la BWANA [“Yehova,” NW], Mungu wako.” (Kutoka 20:7) Hata hivyo, sarafu hizi zatoa ushahidi kwamba jina la kimungu, Yehova, limejulikana na watu katika Ujerumani kwa muda mrefu. Je, unamjua vema jinsi gani Mungu mwenye jina hilo?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki