Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w95 7/1 uku. 32
  • “Kupita Mipaka ya Utimamu wa Akili”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Kupita Mipaka ya Utimamu wa Akili”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
w95 7/1 uku. 32

“Kupita Mipaka ya Utimamu wa Akili”

“KWA kuwa vita huanza katika akili za watu, ni katika akili za watu tunamohitaji kujenga nguzo za amani.” (Sera ya Shirika la UM la Elimu, Sayansi, na Tamaduni) Tukifikiria sera hiyo, katika 1993 zaidi ya wastadi 500 waliokuwa wakihudhuria kongamano la UM juu ya kupunguzwa kwa silaha walijadili fungu la dini katika kujenga nguzo hizo.

Jonathan Granoff, akiwakilisha Muungano wa Mawakili Kwa Ajili Ya Usalama wa Ulimwengu, alikuwa msimamizi wa kongamano hilo. Yeye alisema: “Mweneo wa mapigano ya sasa ya kidini na kikabila unapita kwa mbali mwenendo wa ustaarabu, wawezekana hata kupita mipaka ya utimamu wa akili.” Maneno ya John Kenneth Galbraith yalinukuliwa ifaavyo katika kongamano hilo: “Watu wengi zaidi wameuawa kwa jina la dini kuliko vita vyote na misiba yote ya asili zikijumlishwa pamoja.”

Dakt. Seshagiri Rao alisema: “Matabibu hutakiwa kutibu si kueneza maradhi. Mapokeo ya kidini hayatakiwi kueneza chuki na mapigano ya kijeuri. Hayo hutakiwa kuwa kani za kuleta upatano. Lakini, kihalisi, mara nyingi hayo hutumika na yangali yanatumika kuwa kani za kuleta mizozo.”

Miaka kadhaa iliyopita, gazeti Catholic Herald la London lilieleza kwamba amani yaweza kuhakikishwa tu “ikiwa makanisa ya leo yangeshutumu pamoja vita.” Hata hivyo, gazeti hilo lilitaja: “Twajua kwamba hili halitatendeka kamwe.” Mtawa wa kike wa Kikatoliki alisema hivi: “Ulimwengu ungekuwa tofauti kama nini ikiwa sisi sote tungeamka asubuhi moja tukiwa tumeazimia kabisa kutochukua silaha tena, . . . kama tu Mashahidi wa Yehova!”

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 32]

Tom Haley/Sipa Press

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki