Je, Mungu Anatawala Ulimwengu?
NI Jumapili asubuhi. Watu wengi hushuka kitandani, huvaa, hula kiamsha kinywa, na kwenda haraka kanisani. Huko wasikia mahubiri juu ya jinsi Mungu hutawala juu sana juu ya dunia, akiwa na mamlaka yasiyolinganika. Waambiwa kwamba yeye hujali sana watu. Yesu Kristo amerejezewa pia. Huenda wakasikia kwamba yeye ni Mfalme wa wafalme ambaye kwake kila goti hupigwa kwa utiifu.
Warudipo nyumbani kutoka kanisani, watu hawa huenda wakafungua televisheni na kusikiliza habari. Sasa wanasikia juu ya njaa kuu, uhalifu, uzoefu wa dawa za kulevya, umaskini. Huku wakitazama hali zenye kusikitisha za maradhi na kifo.
Watu hao huenda wakaanza kushangaa juu ya yale waliyosikia kanisani na hasa juu ya mambo yasiyofafanuliwa kamwe huko. Ikiwa Mungu ni mwenye upendo na mwenye nguvu zote, kwa nini mambo mabaya hufanyika? Na vipi juu ya Yesu Kristo? Bila shaka, kuna magoti mengi yasiyopigwa kwa kumtii.
[Picha katika ukurasa wa3]
Ikiwa Mungu hutawala ulimwengu, kwa nini kuna mateseko na msukosuko kama huu?
[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 2]
Jalada: Picha ya NASA