Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w95 8/15 uku. 32
  • Kitulizo kwa Majeruhi Wasio na Hatia

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kitulizo kwa Majeruhi Wasio na Hatia
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
w95 8/15 uku. 32

Kitulizo kwa Majeruhi Wasio na Hatia

NI MOJAPO uhalifu wenye kuchukiza sana uliowahi kutendwa na mwanadamu—kutoa watoto dhabihu kidesturi. Watu fulani hawaamini kwamba zoea baya kama hilo laweza kuwa lilitendeka. Lakini tabia hiyo ya ibada ya Wafoinike imethibitishwa na mavumbuzi mengi ya kiakiolojia.

Watoto kutoka kwa familia za hali ya juu walitolewa kuwa dhabihu kwa miungu kama vile Tanit na Baal-Hammon. Katika Carthage watoto wasio na hatia walitolewa dhabihu kwa sanamu ya shaba ya Kronos. Diodorus Siculus, mwanahistoria wa karne ya kwanza K.W.K., asema kwamba watu wa ukoo wa mtoto huyo hawakuruhusiwa kulia. Labda iliaminiwa kwamba machozi ya huzuni yangepunguza thamani ya dhabihu hiyo.

Kipindi fulani, desturi kama hiyo ilifanywa karibu na Yerusalemu katika Tofethi ya kale. Huko waabudu wangecheza dansi na kupiga vinubi ili wasiweze kusikia kilio cha mtoto alipotupwa katika tumbo la Moleki la tanuru.—Yeremia 7:31.

Yehova huhisi hasira nyingi kuelekea wale ambao huziba masikio yao bila huruma wasisikie kilio cha wenzao. (Linganisha Mithali 21:13.) Akiwa Mungu aonyeshaye huruma kwa watoto, bila shaka Yehova atawafufua watoto hao wasiokuwa na hatia katika ‘ufufuo wa wafu, wa wenye haki na wasio haki pia.’—Matendo 24:15; Kutoka 22:22-24.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki