Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w95 11/1 uku. 32
  • ‘Kama Vile Chuma Kinoavyo Chuma’

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • ‘Kama Vile Chuma Kinoavyo Chuma’
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
w95 11/1 uku. 32

‘Kama Vile Chuma Kinoavyo Chuma’

KUELEKEA mwisho wa karne ya tatu W.K., mwanamume mchanga mwenye bidii aliyeitwa Anthony, aliyefafanuliwa kuwa “Mkristo Mkoptiki,” aliacha kuishi na watu na kuishi miaka 20 peke yake jangwani. Kwa sababu gani? Alihisi kwamba hii ilikuwa ndiyo njia bora kwake ya kumtumikia Mungu. Alikuwa mkaa-pekee wa kwanza wa Jumuiya ya Wakristo mwenye uvutano mwingi.

Leo Jumuiya ya Wakristo ina wakaa-pekee wachache. Lakini watu wengi zaidi na zaidi hutafuta kujitenga kwa njia nyingine. Wao hukataa kuzungumza na wengine juu ya dini, wakihisi kwamba mazungumzo kama hayo huongoza kwenye mabishano na magombano. Jambo kuu katika ibada yao ni kutodhuru jirani yao.

Kweli, kutodhuru jirani ni sehemu moja ya ibada ya kweli, lakini mengi yanahitajiwa. Mithali ya kale husema: “Chuma hunoa chuma; ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake.” (Mithali 27:17) Uhakika ni kwamba Biblia hutia Wakristo moyo kukutana pamoja, wasiache kuishi na watu kabisa au kujitenga na Wakristo wengine. (Yohana 17:14, 15) Yasema hivi: “Tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri; wala tusiache kukusanyika pamoja.” (Waebrania 10:24, 25) Mashahidi wa Yehova hufuata shauri hilo. Wao hukutana pamoja mara kadhaa katika juma ili ‘kunoana uso,’ wakijenga imani ya waamini wenzao. Wao hupata kuona kwamba kuzungumza juu ya Biblia kwa unyofu hakuongozi kwenye magombano. Bali, huongoza kwenye muungano na amani. Kufanya hivyo ni sehemu kuu ya ibada ya kweli.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki