Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w96 1/15 uku. 30
  • Maendeleo Makubwa ya Kisheria

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maendeleo Makubwa ya Kisheria
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
w96 1/15 uku. 30

Maendeleo Makubwa ya Kisheria

KATIKA Aprili ya 1995, kulikuwa na ushindi mkubwa wa mahakama. Hayo yote yalianza Januari 28, 1992, wakati Luz Nereida Acevedo Quiles, mwenye umri wa miaka 24, alipolazwa katika Hospitali ya El Buen Pastor katika Puerto Riko afanyiwe upasuaji usio wa lazima. Alipolazwa tu, alisema kwa maneno na kwa maandishi kwamba akiwa mmoja wa Mashahidi wa Yehova, hangekubali kutiwa damu mshipani. (Matendo 15:28, 29) Wafanyakazi wa hospitali waliohusika, kutia ndani daktari aliyekuwa akimtibu, walijua vizuri matakwa yake.

Siku mbili baada ya kufanyiwa upasuaji, Luz alipoteza damu nyingi sana hata akawa na upungufu mkubwa wa damu kwa sababu ya mvujo. Tabibu aliyekuwa akimtibu, Dakt. José Rodríguez Rodríguez, aliamini kwamba njia ya pekee ya kumsaidia ilikuwa kumtia damu mshipani. Basi, bila Luz kujua na bila idhini yake, tabibu huyo alitafuta amri ya mahakama ya kumtia damu mshipani.

Ingawa Luz alikuwa na ufahamu kabisa naye angeweza kujisemea mwenyewe, Dakt. Rodríguez Rodríguez alisisitiza kwamba kwa sababu ya udharura wa hali yake, hakukuwa na wakati wa kutafuta kibali cha mtu yeyote. Wakili wa mashtaka wa wilaya, Eduardo Pérez Soto, alitia sahihi fomu hiyo, naye hakimu wa wilaya, Mheshimiwa Ángel Luis Rodríguez Ramos, alitoa amri ya mahakama atiwe damu mshipani.

Hivyo, Januari 31, 1992, Luz alipelekwa chumba cha upasuaji, ambamo alitiwa damu mshipani. Wakati wa kutiwa damu mshipani, alisikia wafanyakazi wengine wa hospitali wakicheka. Wengine walimkemea, wakisema kwamba kile alichokuwa akifanyiwa kilikuwa cha manufaa kwake. Alipigana kwa uwezo wake wote—bila mafanikio. Kufikia mwisho wa siku, Luz alikuwa amepokea painti nne za damu.

Kisa cha Luz hakikuwa cha kwanza wala cha mwisho kuhusu utiaji-damu mishipani kwa Mashahidi wa Yehova katika Puerto Riko. Kabla ya kisa chake, angalau amri 15 za mahakama za utiaji-damu mishipani zilikuwa zimetolewa dhidi ya matakwa ya Mashahidi wa Yehova walio watu wazima, na nyingine zaidi zimetolewa tangu wakati huo. Kwa kuhuzunisha, katika kisa kimoja amri ya mahakama ilitekelezwa, na mgonjwa akatiwa damu mshipani kwa nguvu alipokuwa amepoteza ufahamu.

Hata hivyo, pigano la Luz halikumalizika katika chumba cha upasuaji. Mnamo Oktoba 1993 mashtaka yalipelekwa mahakamani dhidi ya Serikali ya Puerto Riko. Kesi ilisikizwa na Mahakama ya Juu, na Aprili 18, 1995, uamuzi wa kupendelea Luz ulifikiwa. Mahakama ilisema kwamba amri ya utiaji-damu mshipani “haikuwa halali nayo ilimnyima mlalamishi haki yake ya kuwa na uhuru wa kidini, ufaragha wake na azimio lake juu ya mwili wake bila sheria kufuatwa.”

Uamuzi huo ulikuwa wa maana, kwa kuwa hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwamba mahakama katika Puerto Riko ilikuwa imeamua kwa kupendelea Mashahidi wa Yehova katika kesi kuhusu utiaji-damu mishipani. Hukumu hiyo ilitokeza itikio kubwa sana. Mkutano wa waandishi wa habari ulifanywa, huku waandikaji na watangazaji wa habari wa magazeti, redio, na televisheni walio maarufu wakiwepo.

Usiku uo huo programu fulani ya redio ilitangaza mahoji ya mmoja wa mawakili wa Luz. Wasikilizaji waliombwa wapige simu na kuuliza maswali. Madaktari na mawakili wengi walipiga simu na kuonyesha walikubaliana na uamuzi wa kesi hiyo. Mpiga-simu mmoja alisema: “Sayansi haijaweza kuthibitisha kwamba utiaji-damu mishipani utaokoa uhai, na ni udanganyifu kufikiri hivyo.” Pia alisema hivi: “Karibuni, utiaji-damu mishipani utawekwa katika rekodi za historia kuwa mojapo mapotovu na makosa makubwa zaidi ya tiba ya kisasa.”

Profesa mmoja wa sheria aliye mashuhuri sana baadaye alipigia simu ofisi ya tawi ya Watch Tower Society na kuonyesha uradhi wake wa kina kwa kile alichotaja kuwa “ushindi mkubwa.” Aliongezea kwamba uamuzi huo wa mahakama watetea haki za kikatiba, si ya Mashahidi wa Yehova pekee, bali ya wananchi wote wa Puerto Riko.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki