Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w96 1/15 uku. 32
  • Mwabudu Yehova kwa Mikono Safi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mwabudu Yehova kwa Mikono Safi
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
w96 1/15 uku. 32

Mwabudu Yehova kwa Mikono Safi

AKIWA amepuliziwa, mtunga-zaburi Daudi aliimba hivi: “Nitanawa mikono yangu kwa kutokuwa na hatia, na kuizunguka madhabahu yako, Ee BWANA.”—Zaburi 26:6.

Katika kutunga maneno hayo, huenda Daudi alikuwa akirejezea desturi ya makuhani Walawi wa Israeli ya kupanda jukwaa la madhabahu na kisha kuweka dhabihu zao juu ya moto. Lakini kabla ya kufanya tendo hili la ibada, makuhani waliamriwa kuosha mikono na miguu yao. Hilo halikuwa jambo dogo lisilo na maana. Kukosa kuchukua hatua hiyo ya kwanza kuliweza kumgharimu kuhani uhai wake!—Kutoka 30:18-21.

Kuosha kitamathali hutokeza usafi wa kiroho na kiadili. (Isaya 1:16; Waefeso 5:26) Yehova atutaka ‘tuizunguke madhabahu yake’ leo kwa kumtumikia. Lakini yeye ataka tufanye hivyo kwa mikono safi—kama Daudi alivyotaja, mikono inayosafishwa “kwa kutokuwa na hatia.” Hili si takwa dogo, kwa kuwa wale ambao huzoea ukosefu wa usafi hawataurithi Ufalme wa Mungu. (Wagalatia 5:19-21) Maisha katika kazi za kimungu haimpi mtu ruhusa ya kushiriki katika mwenendo usio wa adili. Kwa hiyo mtume Paulo aliandika hivi: “Nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.”—1 Wakorintho 9:27.

Wale ambao hutafuta kibali cha kimungu na furaha ya kweli ni lazima wamtumikie Yehova kwa mikono safi. Kama Daudi, wao hutembea “kwa ukamilifu wa moyo, na kwa adili.”—1 Wafalme 9:4.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki