Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w96 2/15 uku. 32
  • Kweli ya Gospeli

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kweli ya Gospeli
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
w96 2/15 uku. 32

Kweli ya Gospeli

VIPANDE vitatu vidogo sana vya hati-kunjo fulani ya Gospeli ya Mathayo, iitwayo P64, vimemilikiwa na Chuo cha Magdalen katika Oxford, Uingereza, tangu 1901. Kwa muda fulani, wasomi waliamini kwamba hivyo vilikuwa vya sehemu ya mwisho-mwisho ya karne ya pili W.K.

Majuzi, Carsten P. Thiede, mstadi wa elimu ya mafunjo katika Paderborn, Ujerumani, alifanya uchunguzi wa kina sana kwa P64, ambayo ina visehemu vya mistari 10 kutoka Mathayo sura ya 26. Tokeo likawa nini? Akiandika katika Zeitschrift für Papyrologie und Epigraphik (Jarida la Elimu ya Mafunjo na Epigrafia), Thiede afafanua vipande vya Oxford kuwa “kipande cha kodeksi ya Kikristo cha karne ya kwanza, labda (ingawa si lazima) kikiwa cha kabla ya mwaka 70 WK.”

Maoni ya Thiede yalijadiliwa sana katika vyombo vya habari na miongoni mwa wasomi. Kwa nini? Kwa sababu kile ambacho sasa hukubaliwa kuwa sehemu ya andiko ya kale zaidi inayobaki ya zile Gospeli ni P52, ambacho ni kipande cha Gospeli ya Yohana cha tangu karibu 125 W.K., au si mapema zaidi kuliko karne ya pili.

Haijulikani kama hiyo tarehe mpya iliyopewa vipande vya mafunjo P64 itakubaliwa na wengi. Kwa vyovyote vile, tarehe ya mapema zaidi haiwezi tu kufanya P64 iwe vipande vya Gospeli vya kale zaidi; bali pia ingetoa uthibitisho zaidi unaoonyesha kwamba Gospeli ya Mathayo kwa kweli iliandikwa katika karne ya kwanza, labda hata kabla ya 70 W.K., wakati ambapo watu wengi waliojionea matukio ya maisha ya Yesu walipokuwa wangali hai ili kuthibitisha kweli ya Gospeli.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 32]

Kwa ruhusa ya Msimamizi na Washiriki wa Chuo cha Magdalen, Oxford.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki