Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w96 10/1 uku. 32
  • Gazeti Linalougusa Moyo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Gazeti Linalougusa Moyo
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
w96 10/1 uku. 32

Gazeti Linalougusa Moyo

MAGAZETI yasiyohesabika yanatangazwa kotekote tufeni ili kutosheleza njaa ya msomaji ya kupata habari au vitumbuizo.

Ni jambo gani linalofanya gazeti lililo mkononi mwako liwe lenye kutokeza sana? Barua ifuatayo, iliyopokewa na ofisi ya tawi ya Watch Tower Society katika Ujerumani, huenda ikatoa jibu:

“Asanteni sana, ndugu wapendwa, kwa jitihada na kazi zenu. Wana wangu wawili na mimi tuliporudi kutoka mkutano, ingawa ilikuwa saa 3:30 usiku, nililazimika tu kusikiliza Mnara wa Mlinzi la karibuni zaidi [katika kaseti]. Nilipokuwa nikiosha vyombo, nilianza kusikiliza makala ya funzo ya kwanza (Aprili 1, 1995). Nilihisi kwamba nililazimika kuisikiliza mara nyingine tena, kwa hiyo nilikatiza kazi yangu jikoni, nikasoma makala [“Wewe Ni Mwenye Thamani Machoni pa Mungu!”] katika Mnara wa Mlinzi kwa kuandamana na tepu. Iliugusa moyo wangu, hasa fungu la nne na la tano. Kisha machozi yakaanza kutiririka—lakini si kwa muda mrefu. Namshukuru Yehova kwamba niko hai nami ni mmoja wa watu wake na kwamba mimi, pamoja na wengine wengi sana, twaweza kujulisha jina lake. Kwa kweli hakuna sababu ya kuhisi hatufai kitu. Roho ya Yehova i pamoja na watu wake. Sote na tuvumilie na kusimama imara katika imani, kwa muungano. Kwa shauku ya Kikristo, dada yenu katika imani.”

Mnara wa Mlinzi hutoa mengi zaidi kuliko habari tu. Linaigusa mioyo ya wasomaji walo na kutosheleza tamaa yao ya kupata lishe ya kiroho na kitia-moyo cha wakati unaofaa. Ndiyo, Mnara wa Mlinzi huandaa “chakula kwa wakati wake.”—Mathayo 24:45.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki