Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w96 11/15 uku. 24
  • Haki ya Idhini Baada ya Kuarifiwa Yathibitishwa Tena

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Haki ya Idhini Baada ya Kuarifiwa Yathibitishwa Tena
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
w96 11/15 uku. 24

Haki ya Idhini Baada ya Kuarifiwa Yathibitishwa Tena

HUKUMU ya juzijuzi iliyotangazwa na Hakimu wa Uchunguzi wa Mwanzo-Mwanzo wa Mahakama ya Messina, Italia, imethibitisha tena kwamba mapendezi ya kitiba ya mgonjwa aliye mtu mzima huwafunga madaktari. Hukumu hiyo ilitolewa katika kesi iliyohusisha mmoja wa Mashahidi wa Yehova.

Katika Januari 1994, Antonino Stellario Lentini, Shahidi mwenye umri wa miaka 64 mwenye ugonjwa wa hemofilia, alikimbizwa kwenye hospitali fulani katika Taormina, Messina. Mke wa Antonino, Catena, aliwaeleza wafanyakazi wa hospitali kwamba wakiwa Mashahidi wa Yehova yeye na mumewe wasingekubali matibabu ya kutiwa damu mishipani. (Matendo 15:20, 28, 29) Mapendezi yao yalistahiwa.

Hata hivyo, wakati wa kusafirishwa hadi kituo kingine cha utunzaji wa afya, Antonino alishindwa kupumua naye akafika huko akiwa mahututi. Upesi baada ya hapo, akafa. Catena aliumia sana, lakini alipata faraja kubwa katika ahadi ya Biblia ya ufufuo. (Matendo 24:15) Kisha, kwa mshangao wake mkubwa, mahakimu-wakazi—huenda wakiwa wamepotoshwa na habari zisizo sahihi zilizochochewa na vyombo vya habari—wakamshtaki kwa kusababisha kifo cha mumewe kwa sababu ya kukataa matibabu ambayo madaktari waliona kuwa ya lazima.

Baada ya zaidi ya mwaka mmoja, Julai 11, 1995, Catena aliachiliwa, kwa kuwa hakuwa amefanya uhalifu wowote. Kwa hakika, ushuhuda wa wataalamu ulionyesha kwamba, kwa kufikiria hali ya mgonjwa, kuingilia kwa kitiba kungekuwa kazi bure kwa vyovyote.

Lakini taarifa za hakimu zilifikia suala kuu. Alionyesha kwamba ni vigumu kwa mahakama kukubali lile wazo la kwamba wafanyakazi wa kitiba hawana budi kuingilia wakati ambapo matibabu yamekataliwa na mgonjwa au na watu wanaomwakilisha. Sheria ya maadili ya kitiba katika Italia, akaongeza, “hutangulia kuona lazima ya kupata idhini ya mgonjwa au mwakilishi wa mgonjwa baada ya kumwarifu kabla ya kuingilia.” Hivyo, alitaarifu kwamba Catena “alimzuia kisheria mumewe asitendewe hivyo.”

Hukumu hiyo yathibitisha tena ile haki ya mtu mzima ya kukataa matibabu yanayohitilafiana na mapendezi yake.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki