Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w97 2/1 uku. 32
  • Ushindi Mwingine kwa Mashahidi wa Yehova Katika Ugiriki

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ushindi Mwingine kwa Mashahidi wa Yehova Katika Ugiriki
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
w97 2/1 uku. 32

Ushindi Mwingine kwa Mashahidi wa Yehova Katika Ugiriki

KATIKA Oktoba 6, 1995, kesi ya kisheria iliyohusisha wahudumu wawili wa wakati wote wa Mashahidi wa Yehova ilisikiwa na Mahakama ya Wasimamizi yenye washiriki watatu katika Athene. Mashtaka yalikuwa juu ya kugeuza watu kidini, nayo yalikuwa yametokezwa na ofisa wa polisi baada ya hao Mashahidi kutembelea nyumbani kwake.

Maswali aliyouliza hakimu-msimamizi yalionyesha kwamba alipendezwa sana na kazi ya Mashahidi wa Yehova. Kwa kielelezo, aliuliza hivi: “Mmekuwa mkifanya kazi hii kwa muda gani? Watu wamekuwa wakiwatendeaje kwa miaka yote? Kazi yenu imeitikiwaje? Mnawaambiaje watu mlangoni pao?” Wote waliokuwapo mahakamani walisikiliza kwa makini ushahidi huo mzuri uliotolewa.

Kwa mshangao mkubwa wa Mashahidi, hata wakili wa mashtaka aliwaunga mkono. “Mashahidi wa Yehova wana haki ya kikatiba ya kumwamini na kumwabudu Mungu wao,” akasema katika hotuba yake ya kumalizia, “na pia ya kueneza imani yao nyumba hadi nyumba, katika nyanja za umma, na barabarani, hata kugawanya fasihi zao bila malipo ikiwa wataka kufanya hivyo.” Wakili wa mashtaka alirejezea maamuzi mbalimbali ya kuondolea hatia yaliyotolewa na mahakama mbalimbali na Baraza la Serikali. Hata alirejezea kesi ya Kokkinakis v. Greece, ambayo uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu uliwaunga mkono Mashahidi wa Yehova.a “Tafadhali angalieni,” akaonya wakili wa mashtaka, “kwamba hata serikali ya Ugiriki ililipa faini katika kesi hiyo. Kwa hiyo twapaswa kuwa waangalifu sana tuombwapo kuhukumu kesi za aina hii. Kwa hakika, kesi hizi hazipasi kuletwa mahakamani kamwe.”

Baada ya hotuba ya wakili wa mashtaka, wakili wa Mashahidi hakuhitaji kusema mengi. Hata hivyo, alichukua hiyo fursa kukazia kwamba ile sheria juu ya kugeuza watu kidini si ya kikatiba na kwamba imekuwa ikiaibisha Ugiriki mbele ya mataifa yote.

Hakimu-msimamizi aliwatupia macho tu wale mahakimu wengine wawili, na wote wakakubali kuwaondolea hatia yule ndugu na yule dada. Kesi hiyo, iliyochukua muda wa saa moja na dakika kumi, ilikuwa ushindi kwa jina la Yehova na pia kwa watu wake.

Baada ya ile kesi ya Kokkinakis kusikiwa na Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu, hii ni kesi ya nne kuondolea hatia iliyohusisha mashtaka ya kugeuza watu kidini. Mashahidi wa Yehova katika Ugiriki wanashangilia kwamba matatizo kuhusiana na kuhubiri kwao karibu yametoweka kabisa na kwamba yawezekana kuendelea na hiyo kazi bila kizuizi.

[Maelezo ya Chini]

a Ona Mnara wa Mlinzi, Septemba 1, 1993, kurasa 27-31.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki