Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w97 4/1 uku. 30
  • Ndoa ya Miaka 403 Imo Taabani

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ndoa ya Miaka 403 Imo Taabani
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
w97 4/1 uku. 30

Ndoa ya Miaka 403 Imo Taabani

KATIKA Sweden, Kanisa na Serikali zimekuwa na uhusiano wa karibu kwa miaka zaidi ya 400. Sasa hiyo ndoa kati ya dini na serikali inadhoofika.

Dini ya Lutheri ilifanywa dini ya Serikali mwaka wa 1593, na Wasweden wote walipaswa kuwa washiriki waliobatizwa wa hiyo dini. Miaka kadhaa baadaye, katika miaka ya 1850, rekebisho lilifanywa. Haikuwa lazima tena kwa Wasweden kubatizwa; hata hivyo, bado walionwa kuwa washiriki wa Kanisa la Lutheri. Wakiwa hivyo, walitakwa walipe asilimia 1 ya mapato yao yenye kukodiwa ili kutegemeza kanisa na kulipia utumishi mwingine mbalimbali wa kiraia uliotolewa na kanisa. Majuzi zaidi badiliko jingine lilitukia. Kuanzia mwaka wa 1952, Wasweden waliweza kujitenga na kanisa kisheria na hivyo wasilazimike kulipa kiasi kikubwa cha kodi ya kanisa.

Katika miaka ya majuzi Kanisa la Lutheri limeendelea kupoteza uongozi walo katika Sweden. Hilo halikuweza kuepukika, kwa kuwa asilimia 10 ya wakaao Sweden ni wahamiaji wasio wa Dini ya Lutheri, kutia ndani Wayahudi, Wakatoliki, na Waislamu. Hivyo, mwanzoni mwa mwaka wa 1996, asilimia 86 tu ya Wasweden walikuwa wa la Lutheri, na idadi hiyo yaendelea kupungua.

Ubaridi unaozidi kuongezeka unalazimisha mtengano kati ya Kanisa na Serikali. Tayari, imejulishwa wazi kwamba mfalme hahitaji kuwa wa Dini ya Lutheri, na watoto wa mzazi aliye wa Dini ya Lutheri hawaonwi moja kwa moja kuwa washiriki wa Kanisa la Serikali la Lutheri. Zaidi ya hayo, kulingana na kichapo The Dallas Morning News, kufikia mwaka wa 2000, “ni lazima parokia za mahali hapo na serikali zipime thamani na kugawanya zile mali nyingi zilizo za kanisa sasa. Lazima kanisa lipunguze bajeti yalo ya dola bilioni 1.68 kwa mwaka, ambayo sehemu yalo kubwa inakusanywa kupitia kodi.” Baada ya mwaka wa 2,000, kanisa litajiwekea rasmi maaskofu walo lenyewe.

Ingawa ubaridi na kupungua kwa washiriki kumeikumba Jumuiya ya Wakristo, Mashahidi wa Yehova katika Sweden wanaendelea kusitawi. Kitabu 1997 Yearbook of Jehovah’s Witnesses charipoti kwamba kuna watangazaji 24,487 wa Ufalme wa Mungu nchini humo, na karibu asilimia 10 wanahubiri wakiwa wahudumu mapainia wa wakati wote. Wengi kati yao wanafikia mapendeleo makubwa zaidi ya utumishi. Kwa kielelezo, katika mikusanyiko ya wilaya ya Mashahidi wa Yehova ya mwaka wa 1995, wenzi 20 wa ndoa walitoa maombi yao ya kupata mazoezi ya umishonari kwenye Shule ya Biblia ya Gileadi ya Watchtower. Wakati huo, kulikuwa na wahitimu Wasweden 75 wa madarasa yaliyopita waliokuwa wakitumikia katika utumishi wa umishonari katika sehemu tofauti za ulimwengu. Bila shaka, kielelezo chao chema na barua na ziara zao zenye kutia moyo zina matokeo yenye kuchochea juu ya wale wanaofikiria pendeleo hilo tukufu sasa.

Hivyo, huku mamilioni ya washiriki wa Jumuiya ya Wakristo wapatwapo na uchungu wa roho, Mashahidi wa Yehova ‘wanaimba kwa furaha ya moyo.’—Isaya 65:13, 14.

[Ramani katika ukurasa wa 30]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

Sweden

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki