Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w97 12/1 uku. 32
  • Zile Amri Kumi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Zile Amri Kumi
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
w97 12/1 uku. 32

Zile Amri Kumi

ASKOFU wa Uingereza wa Gloucester aligundua kwamba zaidi ya nusu ya makasisi katika dayosisi yake hawakuweza kukariri zile Amri Kumi, na asilimia 10 ya makasisi hao hawakujua wawezapo kuzipata katika Biblia. Lakini hiyo ilikuwa miaka 450 iliyopita. Je, hiyo hali imeboreka tangu wakati huo? La hasha—kama vile ilivyofunuliwa na uchunguzi wa majuzi usio na utaratibu maalumu wa makasisi Waanglikana uliofanywa na gazeti Sunday Times.

Kati ya wale makasisi 200 waliohojiwa, ni asilimia 34 tu walioweza kutaja Amri Kumi zote. Miongoni mwa waliosalia, mmoja alihisi kwamba zilikuwa na vizuizi vingi mno, na mwingine akasema kwamba hazihusu magumu ya kisasa ya kiadili.

Je, wazijua zile Amri Kumi au wajua uwezapo kuzipata? Zimerekodiwa katika Kutoka, kitabu cha pili cha Biblia, mistari 17 ya kwanza ya sura ya 20. Kwa nini usizisome? Hii ni njia sahili ya kuzipanga katika makundi. Za kwanza nne zahusu kumwabudu kwetu Mungu, ya tano yakazia maisha ya familia, namba sita hadi tisa zahusu uhusiano wetu na binadamu-mwenzetu, na ya kumi ni ya pekee, ikitufanya tuichunguze mioyo yetu wenyewe, tuchunguze nia zetu. Ufuatao ni muhtasari mfupi wa jinsi ambavyo Wakristo huenda wakatumia hizo kanuni.

Ya kwanza: Mpe Muumba wetu ujitoaji usiohusisha wengine. Ya pili: Usitumie mifano katika ibada. Ya tatu: Stahi na kuadhimisha jina la Mungu sikuzote. Ya nne: Ruhusu wakati wa kukazia fikiria mambo ya kiroho, bila kukengeushwa fikira. Ya tano: Watoto, wastahini wazazi wenu. Ya sita: Usiue kimakusudi. Ya saba: Epuka uzinzi. Ya nane: Usiibe. Ya tisa: Sema kweli. Ya kumi: Epuka kabisa kutamani.

Hizo Amri Kumi zilikuwa sehemu ya mfumo wa sheria alizopewa Musa. Lakini kanuni zilizomo ni za sikuzote. (Waroma 6:14; Wakolosai 2:13, 14) Kwa sababu hiyo, wafuasi wa Yesu walinukuu na kurejezea Amri Kumi. (Waroma 13:8-10) Leo maisha yangekuwa yenye furaha zaidi—na salama zaidi—kama nini ikiwa wote wangestahi na kuishi kupatana na kanuni hizi zilizopuliziwa kimungu!

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki