Zamtukuza Muumba Wake Kimya-Kimya
KIASILI machweo ni ya kutazamisha. Lakini kwa kweli ni jambo la kipekee kuona jua likishuka nyuma ya mlima huu mahususi ulioko penye milima ya Apuan Alps ya Tuscany, Italia.
Likitazamwa kutoka mbali, jua huonekana kuwa latumbukia katika mlima badala ya kushuka nyuma yake. Kwa nini? Kwa sababu kilele cha huo mlima kina tao la asili ambalo huonekana kana kwamba lilichimbwa kutoka katika huo mlima. Kwa kweli, rasi hii imejipatia jina, Monte Forato—Mlima Uliotobolewa. Kwa sababu ya mwendo wa dunia kulizunguka jua, ni katika pindi mbili tu kila mwaka ambazo wale wenye kuangalia kupitia hili tao waweza kuona jua ambalo huonekana kana kwamba linatumbukia katika Monte Forato.
Kama sehemu nyingine za uumbaji, mbingu zisizo na uhai humsifu Muumba wake. Jinsi gani? Katika njia ileile ambayo mchoro wa rangi ulio mzuri huenda ukamletea sifa msanii aliyeuchora. Kwa kweli, sayari za juu husema juu ya nguvu, hekima, na ukuu wa Yehova. Kama vile mtunga-zaburi alivyoeleza, “mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, na anga laitangaza kazi ya mikono yake.” (Zaburi 19:1; 69:34) Kwa kuwa jua na sayari nyingine zisizo na uhai zatukuza Muumba wake, yatupasa sisi tumtukuze kwa kadiri kubwa zaidi kama nini!—Zaburi 148:1, 3, 12, 13.