Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w98 5/1 uku. 32
  • Kwa Nini Usiwe Pamoja Nao?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kwa Nini Usiwe Pamoja Nao?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
w98 5/1 uku. 32

Kwa Nini Usiwe Pamoja Nao?

NDJAUKUA ULIMBA ana umri wa miaka 73, na mwaka jana alisafiri umbali wa kilometa zipatazo 450. Alitembea huo umbali wote, na ulimchukua siku 16.

Mwanamume huyu mzee-mzee alifunga safari yake ili kuhudhuria mojawapo ya mikusanyiko ya kila mwaka ya Mashahidi wa Yehova. Baada ya mkusanyiko, akiwa na shangwe tele na akiwa ameimarishwa kiroho, alitembea tena kurudi nyumbani, yaani, kwa siku nyingine 16. Je, jitihada hiyo ilistahili? Naam, bila shaka! Ndjaukua Ulimba amekuwa akifunga safari hiyo kila mwaka kwa miaka kadhaa.

Mwanamume huyu Mwafrika ni mmoja wa watu zaidi ya milioni 15 kutoka nchi zaidi ya 230 waliohudhuria mikusanyiko ya Mashahidi wa Yehova mwaka jana. Bila shaka, wengi wao, hawakuhitaji kutembea kwa siku nyingi ili kufika kwenye mkusanyiko. Wengi wao walifika kwa gari, basi, garimoshi, au ndege. Je, ulikuwa mmoja wao?

Katika 1998, mikusanyiko itaanza kufanywa tena ulimwenguni pote, hasa wakati wa miezi ya kiangazi (au wakati wa majira yenye ukavu). Afya ikimruhusu, yaelekea Ndjaukua Ulimba atafunga safari hiyohiyo ndefu ili kuhudhuria. Yeye na mamilioni ya watu wengine watasikia programu ifaayo, yenye kuimarisha imani, na yenye kutia nguvu. Huo mkusanyiko utakuwa jambo kuu la mwaka, kwa wote watakaohudhuria. Wewe pia wakaribishwa kwa uchangamfu uhudhurie. Mashahidi wa Yehova wa kwenu watafurahi kukuambia mahali pa mkusanyiko ambapo ni karibu zaidi nawe.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki