Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w98 5/15 uku. 32
  • Mwenendo Mzuri Waleta Sifa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mwenendo Mzuri Waleta Sifa
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
w98 5/15 uku. 32

Mwenendo Mzuri Waleta Sifa

GAZETI la habari la Italia La Gazzetta del Mezzogiorno lilipongeza Mashahidi wa Yehova kwa kuchapisha ile makala “Matera—Jiji la Makao ya Kipekee ya Pangoni.” Makala hii ilitokea katika toleo la gazeti la Amkeni! la Julai 8, 1997, ambalo liligawanywa sana katika lugha nyingi. Gazeti Amkeni! kwa sasa latafsiriwa katika lugha 81, na nakala zaidi ya milioni 19 zagawanywa ulimwenguni pote. Hilo gazeti la habari lilieleza kwamba gazeti Amkeni! lilivunja rekodi ya wakati wa kiangazi hiki “kwa habari ya kampeni za kutangaza ili kukuza historia na urithi wa sanaa wa jiji [la Matera].”

Hilo gazeti la habari lilisifu Mashahidi kuhusu “Imani Katika Neno la Mungu” Mkusanyiko wa Wilaya uliofanyiwa Matera katika 1997. Makala hiyo iliandika kwamba Mashahidi waliweza “kupata watu 4,000 kwenye uwanja [wa jiji] uitwao XXI Settembre Stadium, katika kipindi cha katikati cha kiangazi na chini ya jua lenye kuchoma; wamesafisha, wakapaka rangi upya, na kurekebisha mahali hapa pa michezo (hasa vyoo) bila kutoza malipo yoyote, wakilipia gharama za ununuzi wa vitu vya lazima wao wenyewe.”

Mashahidi wa Yehova hujitahidi kuwa majirani wema. (Mathayo 22:37-39) Pia wao hufuata onyo la upole la Kimaandiko: “Dumisheni mwenendo wenu ukiwa bora miongoni mwa mataifa, ili, . . . likiwa tokeo la kazi zenu bora ambazo wamekuwa mashahidi wa kujionea wapate kumtukuza Mungu katika siku ya ukaguzi wake.”—1 Petro 2:12.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki