Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w98 7/15 uku. 24
  • Mkutano wa Kila Mwaka Oktoba 3, 1998

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mkutano wa Kila Mwaka Oktoba 3, 1998
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • Habari Zinazolingana
  • Mkutano wa Kila Mwaka Oktoba 3, 1998
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • Mkutano wa Kila Mwaka Oktoba 7, 2000
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
  • Mkutano wa Kila Mwaka Oktoba 7, 2000
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
  • Mkutano wa Kila Mwaka Oktoba 4, 1997
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
w98 7/15 uku. 24

Mkutano wa Kila Mwaka Oktoba 3, 1998

MKUTANO WA KILA MWAKA wa washiriki wa Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania utafanywa Oktoba 3, 1998, kwenye Jumba la Kusanyiko la Mashahidi wa Yehova, 2932 Kennedy Boulevard, Jersey City, New Jersey. Mkutano wa utangulizi wa washiriki peke yao utafanywa saa 3:15 asubuhi, ukifuatwa na ule mkutano wa ujumla wa kila mwaka saa 4:00 asubuhi.

Washiriki wa Shirika hilo wanapaswa kuijulisha Ofisi ya Mwandishi sasa juu ya badiliko lolote la anwani zao lililotokea mwaka uliopita ili barua zile za kawaida za ujulisho na za uwakilishaji ziweze kuwafikia wakati wa mwezi wa Julai.

Barua za uwakilishaji, watakazopelekewa washiriki pamoja na ujulisho wa mkutano wa kila mwaka, zinapasa kurudishwa ili ziifikie Ofisi ya Mwandishi wa Sosaiti kabla ya Agosti 1. Inampasa kila mshiriki ajaze mambo yote yaliyo katika barua yake ya uwakilishaji na kuirudisha haraka, akitaarifu kama atakuwapo ama hatakuwapo mkutanoni yeye binafsi. Habari zenye kutajwa katika kila barua ya uwakilishaji zinapaswa kuwa wazi juu ya habari hii, kwa kuwa ndizo zitakazotegemewa katika kujua ni nani watakaokuwapo binafsi.

Inatarajiwa kwamba kipindi kizima, kutia ndani ule mkutano rasmi na ripoti mbalimbali, kitamalizwa ifikapo saa 7:00 alasiri au muda mfupi baada ya hapo. Hakutakuwa na kipindi cha alasiri. Kwa sababu nafasi ni ndogo, itawezekana kuingia kwa kuwa na tikiti tu. Hakutakuwa na mpango wa kuunganisha majumba mengine kwa simu ili kuusikia mkutano wa kila mwaka.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki