Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w99 1/1 uku. 32
  • “Warefu Kama Mwerezi wa Lebanoni”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Warefu Kama Mwerezi wa Lebanoni”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
w99 1/1 uku. 32

“Warefu Kama Mwerezi wa Lebanoni”

JUU ya milima maridadi ya Lebanoni humea miti iitwayo Arz Ar-rab, ikimaanisha “Mierezi ya Bwana.” Miti hii mikubwa isiyonyauka, ambayo wakati fulani ilifunika hiyo milima, hutajwa katika Biblia mara 70 hivi—mara nyingi zaidi kuliko mti mwingine wowote.

Yanapoifafanua miti hii yenye fahari ya Lebanoni, Maandiko hutumia maneno kama vile “bora” na “mzuri.” (Wimbo Ulio Bora 5:15; Ezekieli 17:23) Kwa muda mrefu, ukubwa wa mwerezi na udumifu wa mbao zake umeufanya upendwe sana kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na meli na pia kwa kutengeneza fanicha. Harufu nzuri na rangi nyekundu yenye kuchangamsha ya mbao zake huvutia sana, na kiwango cha juu cha utomvu wake huzifanya zisioze na zisishambuliwe na wadudu. Miti hii ni mirefu na mikubwa sana, ikifikia kimo cha meta 37 na kipenyo cha meta 12, na mizizi yake inapenya ndani sana, na ni thabiti. Haishangazi kwamba wasimamizi fulani wa misitu wa kisasa wameifafanua kama “utimilifu wa utukufu wa ulimwengu wa mimea”!

Katika unabii, mwandikaji wa Biblia Ezekieli, alimlinganisha Mesiya na kitawi cha mwerezi, ambacho Mungu mwenyewe hukipanda. (Ezekieli 17:22) Kwa kweli, neno la Kiebrania linalomaanisha “mwerezi” lina chanzo kinachomaanisha “kuwa imara.” Siku hizi, wafuasi wa Mesiya, Yesu Kristo, vivyohivyo wahitaji “[kusimama] imara katika imani, . . . [kukua wawe] wenye uweza,” kama mwerezi mrefu, ulio thabiti. (1 Wakorintho 16:13) Hili laweza kutimizwaje? Kwa kukinza kwa imara mivutano isiyo ya Kikristo na kudumu bila kuondoleka katika mwendo wa uaminifu-maadili na ujitoaji-kimungu. Wale wanaofanya hivyo hufafanuliwa katika Biblia kuwa “waadilifu ambao wanakua kuwa warefu kama mwerezi wa Lebanoni.”—Zaburi 92:12, The New English Bible.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki