Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w99 5/1 uku. 32
  • Ushindi Dhidi ya Lililo Ovu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ushindi Dhidi ya Lililo Ovu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
w99 5/1 uku. 32

Ushindi Dhidi ya Lililo Ovu

“MBONA mbwa mfu huyu amlaani mfalme bwana wangu? Na nivuke, nakusihi, nikaondoe kichwa chake.” Ombi hilo lilitolewa na Abishai, mkuu wa jeshi la Israeli. Lilikuwa jibu lake la hasira aliposikia bwana wake, Mfalme Daudi, akitukanwa kwa chuki na Mbenyamini aitwaye Shimei.—2 Samweli 16:5-9.

Abishai alifuata falsafa inayoungwa mkono na wengi leo—kanuni inayosema kwamba dawa ya moto ni moto. Naam, Abishai alitaka Shimei aadhibiwe kwa kumtukana Daudi.

Lakini Daudi aliitikiaje? Daudi alimzuia Abishai, akisema: “Mwacheni.” Daudi alikinza kwa unyenyekevu kishawishi cha kulipiza kisasi, ingawa hakuwa na hatia kuhusiana na mashtaka ya Shimei. Badala yake, aliacha jambo hilo mikononi mwa Yehova.—2 Samweli 16:10-13.

Daudi alipoanza kutawala tena baada ya kukimbia maasi ya mwana wake ambayo hayakufua dafu, Shimei alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kumsalimu na kumwomba radhi. Kwa mara nyingine, Abishai alitaka kumwua, lakini Daudi akamzuia tena.—2 Samweli 19:15-23.

Katika kisa hiki, Daudi alibainika kuwa mfano unaofaa wa Yesu Kristo, ambaye mtume Petro aliandika hivi kumhusu: “Alipokuwa akitukanwa, hakuwa akitukana kwa kurudisha . . . lakini alifuliza kujikabidhi mwenyewe kwa yeye ambaye huhukumu kwa uadilifu.”—1 Petro 2:23.

Leo, Wakristo hushauriwa wawe ‘wanyenyekevu katika akili, wakiwa hawalipi ubaya kwa ubaya.’ (1 Petro 3:8, 9) Kwa kufuata kielelezo kilichowekwa na Daudi na Yesu Kristo, sisi pia twaweza “kushinda lililo ovu kwa lililo jema.”—Waroma 12:17-21.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki