Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w99 5/15 uku. 32
  • Jeuri—Karibuni Itakwisha Milele!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Jeuri—Karibuni Itakwisha Milele!
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
w99 5/15 uku. 32

Jeuri—Karibuni Itakwisha Milele!

“Jeuri Yahatarisha Taifa”—The New York Times, Marekani.

“Jeuri Nyumbani”—O Globo, Brazili.

“Jeuri Yawakumba Wanawake Ulimwenguni”—The Globe and Mail, Kanada.

VICHWA hivyo vya magazeti ya Amerika Kaskazini na Kusini huonyesha mwelekeo wenye kushtua wa ulimwenguni pote. Kama Shirika la Afya Ulimwenguni lilivyosema hivi majuzi, “jeuri ya namna zote imeongezeka sana katika miongo ya hivi karibuni.”

Fikiria tarakimu kadhaa zenye kushtua:

Mauaji. Katika Amerika ya Latini na Karibea, watu wapatao 1,250 huuawa kijeuri kila siku. Matokeo ni kwamba “katika nusu ya nchi za eneo hilo, uuaji kimakusudi ndio kisababishi namba mbili cha vifo miongoni mwa vijana wenye umri wa miaka kati ya 15 na 24.”

Jeuri dhidi ya watoto. Matatizo ya kutenda watoto vibaya kimwili, kingono, na kihisia-moyo yameenea ulimwenguni pote. Kwa mfano, “uchunguzi mbalimbali unaohusu watu wazima katika nchi kadhaa zilizoendelea kiviwanda unadokeza kuwa asilimia 10 hadi asilimia 15 ya watoto wametendwa vibaya kingono—wengi wao wakiwa wasichana.”

Jeuri dhidi ya wanawake. Baada ya kuchunguza uvunjaji wa haki za kibinadamu uliotendeka ulimwenguni pote mwaka wa 1997, watafiti walikata kauli kuwa “jeuri ya nyumbani imekuwa mojawapo wa visababishi vikuu vya kujeruhiwa kwa wanawake katika karibu kila nchi ulimwenguni pote.” (Human Rights Watch World Report 1998) Jeuri ya nyumbani, ambayo ni tatizo lililoenea sana lakini linaloripotiwa mara chache, sasa inaitwa “mgogoro wa kimyakimya wa karne ya 20.”—The Globe and Mail, Kanada.

Katika siku za Noa, vivyo hivyo dunia “i[li]jaa dhuluma [“jeuri,” NW].” (Mwanzo 6:9-12) Lakini Yehova Mungu alimhifadhi huyo “mhubiri wa uadilifu” na familia yake “alipoleta gharika juu ya ulimwengu wa watu wasioogopa Mungu.” Vivyo hivyo, Mungu atachukua hatua kama hiyo siku yetu. Atawahifadhi “watu wenye ujitoaji-kimungu” anapowaondoa watu wenye jeuri na waovu na kuifanya hii dunia iwe paradiso katika ulimwengu wake mpya ulioahidiwa. (2 Petro 2:4-9; 3:11-13) Je, wewe husisimuki kujua kuwa karibuni jeuri itakwisha milele?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki