Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w99 8/1 uku. 32
  • Ubaguzi wa Rangi na Dini

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ubaguzi wa Rangi na Dini
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
w99 8/1 uku. 32

Ubaguzi wa Rangi na Dini

NILIPOKUJA Marekani mwaka wa 1978, niliamini kwamba Marekani ilikuwa imetatua matatizo ya kijamii kitambo sana, kwamba watu weusi walikuwa raia sawa na wengine,” akasema Mark Mathabane, mwandishi mzaliwa wa Afrika Kusini, alipohojiwa na gazeti Time. “Katika njia nyingi, niliona jambo hilo kuwa kweli. Marekani ilionekana kuwa imeendelea sana kuliko Afrika Kusini. Kisha nikagundua kwa kuchukizwa kwamba, hakukuwa na badiliko kubwa mioyoni mwa watu.” Ni nini kilichomfanya achukizwe hivyo?

“Wakati ambapo kunakuwa na ubaguzi zaidi Marekani ni Jumapili saa 5:00 asubuhi,” akasema Mathabane. Aligundua kwamba hata kanisani, watu hawawezi kujiunga katika ibada na wale wa jamii nyingine. “Wanaweza kuhisije zile siku nyingine za juma?” akauliza. Akisema juu ya elimu kuwa ndicho kichocheo cha badiliko, Mathabane alisema hivi: “Ukiwa na elimu unafanywa ukubali usawa wa wanadamu.”

Mashahidi wa Yehova wanakubali kwamba elimu ndiyo suluhisho, lakini wanapendekeza hasa elimu inayotegemea Neno la Mungu. Naam, Biblia huwasaidia kuvunjilia mbali vizuizi vya ubaguzi wa rangi—hata katika nchi ambamo chuki ya kikabila imeenea pote. Kila juma katika Majumba yao ya Ufalme, watu wa jamii na mataifa mbalimbali hukusanyika pamoja kuelimishwa katika sheria na kanuni za Neno la Mungu, Biblia. Hakuna sadaka zinazokusanywa katika mikutano hiyo. Unakaribishwa kuhudhuria!

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki