Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w99 8/15 uku. 32
  • “Ikiwa Chumvi Yapoteza Nguvu Yayo”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Ikiwa Chumvi Yapoteza Nguvu Yayo”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
w99 8/15 uku. 32

“Ikiwa Chumvi Yapoteza Nguvu Yayo”

VITA vimepiganwa kwa sababu ya chumvi. Imetumiwa ikiwa kibadilishio. Katika China ya kale, dhahabu tu ndiyo iliyoishinda kwa thamani. Naam, chumvi imeonwa na wanadamu kuwa bidhaa yenye thamani sana. Hadi leo hii, chumvi yaonwa kuwa na uwezo wa kuponya na kuzuia kukua kwa bakteria, nayo hutumiwa ulimwenguni kote ikiwa kikolezo na kihifadhi.

Kwa kuzingatia sifa zenye kupendeza na matumizi mengi ya chumvi, si ajabu kwamba hiyo hutumiwa kwa njia ya kitamathali katika Biblia. Kwa mfano, Sheria ya Kimusa ilitaka kwamba chochote kilichotolewa madhabahuni kwa ajili ya Yehova, kitiwe chumvi. (Mambo ya Walawi 2:13) Hilo halikufanywa ili kuongeza ladha ya dhabihu, bali yaelekea lilifanywa kwa sababu chumvi iliwakilisha kutokuwepo kwa uchafu na uozo.

Katika Mahubiri yake ya Mlimani yaliyo maarufu, Yesu Kristo aliwaambia wafuasi wake: “Nyinyi ndio chumvi ya dunia.” (Mathayo 5:13) Kwa taarifa hiyo, Yesu alidokeza kwamba kuwahubiria wengine juu ya Ufalme wa Mungu kungekuwa na uvutano uwezao kuhifadhi au kuokoa uhai kwa wanaowasikiliza. Kwa kweli, wale waliotumia maneno ya Yesu wangelindwa wasipatwe na uozo wa kiadili na wa kiroho uliokuwamo katika jumuiya walimoishi na kutumikia.—1 Petro 4:1-3.

Hata hivyo, Yesu aliendelea kutoa onyo hili: “Lakini ikiwa chumvi yapoteza nguvu yayo, . . . si yenye kutumika tena kwa kitu chochote bali ni ya kutupwa nje ili kukanyagwa-kanyagwa na watu.” Akieleza juu ya hilo, msomi wa Biblia Albert Barnes alisema kwamba chumvi ambayo Yesu na mitume wake walijua “ilikuwa chafu, imechanganyika na mimea na udongo.” Hivyo, chumvi ikipoteza nguvu yake, “kiasi kikubwa cha udongo” kingebaki. “Huo,” akasema Barnes, “haukufaa chochote ila tu . . . kuuweka kwenye njia, au vijia, kama vile tutumiavyo changarawe.”

Kwa kuzingatia onyo hilo, Wakristo wapaswa wawe waangalifu wasiache kuhubiri hadharani au kurudia mienendo yao miovu. La sivyo, watadhoofika kiroho, wasifae chochote, kama vile ‘chumvi iliyopoteza nguvu yake.’

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki