Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w99 10/15 uku. 32
  • “Moyo Thabiti Uliochochewa na Imani”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Moyo Thabiti Uliochochewa na Imani”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
w99 10/15 uku. 32

“Moyo Thabiti Uliochochewa na Imani”

KATIKA mwaka wa 1998 kitabu kipya cha Kifaransa kiitwacho Les Témoins de Jéhovah face à Hitler (Mashahidi wa Yehova Wakabiliana na Hitler), kilichoandikwa na Guy Canonici, kilitolewa na kusifiwa sana na wachambuzi. Katika dibaji yake kuhusu kitabu hicho, mwandishi mwanahistoria Mfaransa mwenye kustahiwa sana, François Bédarida, aliandika: “Hiki ni kitabu kilichopendwa sana. Siyo kwa sababu kinaziba pengo fulani, bali kwa sababu kiliandikwa kwa wakati ufaao. . . . Mbali na wataalamu, ni nani mwingine ajuaye janga lililowapata Mashahidi wa Yehova chini ya Utawala wa Nazi? Hata hivyo, walinyanyaswa mfululizo na kwa ukatili katika muda wote wa miaka 12 wa utawala huo. Walipatwa pia na mambo yenye kutisha katika kambi za mateso. Waliteswa sana pia kwa sababu ya imani na itikadi zao. Kwa nini historia imewasahau Wakristo hawa? . . .

“Kwa nini dini hiyo ndogo ambayo imetawanyika na isiyodhuru ilinyanyaswa kikatili hivyo? Hilo ndilo jambo la kushangaza. Idadi ya Mashahidi nchini Ujerumani ilikuwa ndogo sana—takwimu zaonyesha walikuwa 20,000 wakilinganishwa na zaidi ya wakazi milioni 60—lakini wote walikuwa raia wenye amani, wenye kufuata sheria na wasiotisha mtu yeyote, ambao walitaka tu kufanya kazi na kulea watoto wao ifaavyo. . . .

“Mnyanyaso huo ulikabili ukinzani wa kiroho ulio thabiti na wenye ushindi kutoka kwa waamini ambao, kupitia nguvu za ndani za imani yao katika Yesu Kristo, waliweza kupambana na mikazo kutoka kwa wanyanyasi, wakikabili kwanza jeuri ya kimwili waliyofanyiwa na Utawala wa polisi—hadi kufikia kuwa mashujaa na wafia-imani.”

Kisa cha Mashahidi wa Yehova waliofia imani yao ya Kikristo huku wakikabiliwa na upinzani wa kidini chavutia sana. Gazeti maarufu la Kifaransa la Katoliki, La Croix, liliongeza kusema hivi katika uchambuzi wake wa kitabu hicho: “Kuhusu historia yao isiyojulikana sana, Guy Canonici amekusanya uthibitisho mwingi ambao humstaajabisha mtu anapoona moyo thabiti uliochochewa na imani iliyofafanuliwa kwa maneno sahili zaidi, imani ambayo ilikuwa thabiti hadi mwisho, hata miongoni mwa watoto. Kumbukumbu hiyo yapaswa kuandaa msingi kwa ajili ya mjadala unaoendelea sasa kuhusu hali ya Ukristo ya Mashahidi wa Yehova.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki