Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w00 2/1 uku. 32
  • Yehova Atakukumbukaje?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yehova Atakukumbukaje?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
w00 2/1 uku. 32

Yehova Atakukumbukaje?

‘UNIKUMBUKE, Ee Mungu wangu.’ Kwa mara kadhaa, Nehemia alimwomba Mungu kwa bidii kwa maneno hayo. (Nehemia 5:19; 13:14, 31) Ni jambo la kawaida kabisa kwa watu kumgeukia Mungu kwa maneno kama hayo ya kusihi wanapopatwa na matatizo.

Hata hivyo, watu hufikiria nini wanapomwomba Mungu awakumbuke? Ni wazi kwamba wao hutumaini kwamba Mungu atafanya mengi zaidi ya kuyakumbuka tu majina yao. Yaelekea wana matumaini kama ya mmojawapo wa wahalifu ambao waliuawa pamoja na Yesu. Mhalifu huyo, tofauti na yule mwingine, alimsihi Yesu hivi: “Nikumbuke mimi uingiapo katika ufalme wako.” Alitaka Yesu akumbuke yeye alikuwa nani na pia amfanyie jambo fulani—amfufue.—Luka 23:42.

Biblia huonyesha daima kwamba Mungu ‘hukumbuka’ kwa kuchukua hatua. Kwa mfano, baada ya dunia kugharikishwa kwa siku 150, “Mungu akamkumbuka Nuhu . . . , Mungu akavumisha upepo juu ya nchi, maji yakapungua.” (Mwanzo 8:1) Karne kadhaa baadaye, Samsoni, akiwa amepofushwa na kufungwa kwa minyororo na Wafilisti, alisali hivi: “MUNGU, unikumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu.” Yehova alimkumbuka Samsoni kwa kumpa nguvu zipitazo za kibinadamu ili aweze kujilipizia kisasi dhidi ya adui za Mungu. (Waamuzi 16:28-30) Kwa habari ya Nehemia, Yehova alibariki jitihada zake, na ibada ya kweli ikarudishwa Yerusalemu.

“Mambo yote yaliyoandikwa wakati wa mbele yaliandikwa kwa kufunzwa kwetu, ili kupitia uvumilivu wetu na kupitia faraja kutokana na Maandiko tupate kuwa na tumaini,” akaandika mtume Paulo. (Waroma 15:4) Tukimkumbuka Yehova kwa kujitahidi kufanya mapenzi yake, kama ambavyo watumishi wake walifanya zamani, tunaweza kuwa na hakika kwamba Yehova atatukumbuka kwa kutusaidia kukidhi mahitaji yetu ya kila siku, kwa kututegemeza katika majaribu, na kwa kutuokoa wakati aletapo hukumu juu ya watu wasiomcha Mungu.—Mathayo 6:33; 2 Petro 2:9.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki