Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w00 3/1 uku. 32
  • Kilirudisha Pete Kwenye Vidole Vyao

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kilirudisha Pete Kwenye Vidole Vyao
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
w00 3/1 uku. 32

Kilirudisha Pete Kwenye Vidole Vyao

“TAZAMA vidole vyangu. Je, unaona tofauti yoyote?” Mwanamume mmoja alinyosha mkono wake kumwonyesha mwanamke mmoja Shahidi wa Yehova, ambaye aliutazama na mara moja akaona kwamba hakuwa na pete yake ya arusi. Mwanamume huyo alieleza kwamba yeye na mke wake wameamua kupata talaka kwa kuwa hawaelewani. “La!” Shahidi huyo akasema. “Chukua kitabu hiki ukasome. Kitakusaidia katika ndoa yako.” Hivyo, akampa kitabu Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele kinachotegemea Biblia.a

Siku kadhaa baadaye mwanamume huyo alirudi kwa Shahidi huyo akiwa mwenye furaha. Akamwonyesha mkono wake. Wakati huu alikuwa amevaa pete yake ya arusi. Alimwambia kwamba yeye na mke wake walikuwa wamekisoma kitabu Ujuzi na kwamba sasa walikuwa wenye furaha sana. Kitabu hicho kilikuwa kimerudisha pete kihalisi kwenye vidole vyao.

Shauri la Biblia linaweza kusaidia mume na mke wapendane kikweli. Inakuwa hivyo kwa sababu Muumba wetu ambaye ndiye mtungaji wa Biblia husema: “BWANA, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.”—Isaya 48:17.

[Maelezo ya Chini]

a Kimechapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki