Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w00 3/15 uku. 32
  • Anachokumbuka Kuhusu New York City

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Anachokumbuka Kuhusu New York City
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
w00 3/15 uku. 32

Anachokumbuka Kuhusu New York City

MAANDISHI yanayoonekana hapa yameonyeshwa waziwazi kwenye mojawapo ya majengo ya kiwanda ya Watchtower Society huko Brooklyn, New York, tangu miaka ya 1950. Wasafiri, watalii, na watu wengineo wanaopita karibu na jengo hilo hukumbushwa kusoma Biblia kila siku. Barua ifuatayo iliyopokewa kutoka kwa msichana mchanga Shahidi, yaonyesha matokeo mazuri ya maandishi hayo.

“Nilikuwa nikizungumza na mwanafunzi wa darasa letu juu ya mambo ambayo ningependa kufanya nikimaliza shule ya sekondari. Nilianza kuzungumza juu ya Betheli, makao makuu ya Mashahidi wa Yehova, naye akasisimuka sana. Aliniambia kwamba aliishi New York City maisha yake yote. Familia yake haikuchukua dini kwa uzito, lakini kila asubuhi alipotazama nje ya dirisha, aliona maandishi yaliyosema ‘Soma Neno la Mungu Biblia Takatifu Kila Siku.’ Hivyo yeye alisoma Biblia yake kila siku kabla ya kwenda shuleni.

“Alisema kile anachokumbuka kuhusu New York City baada ya kuhama huko ni kwamba anapoamka, yeye haoni maandishi hayo yenye kumkumbusha asome Biblia. Lakini kwa sababu ya maandishi hayo kwenye jengo hilo la Watchtower, amekuwa na mazoea ya kusoma Biblia, naye anaendelea kuisoma Biblia kila siku!”

Kusoma sehemu fulani ya Neno la Mungu ni njia bora kama nini ya kuanza siku! Kwa kufanya hivyo, hapana shaka kwamba utakubaliana na maneno haya ya mtume Paulo: ‘Maandishi matakatifu yanaweza kukufanya uwe mwenye hekima kwa ajili ya wokovu kupitia imani kuhusiana na Kristo Yesu.’—2 Timotheo 3:15-17.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki