Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w00 4/15 uku. 32
  • Upaji Wenye Thamani Machoni pa Yehova

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Upaji Wenye Thamani Machoni pa Yehova
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
w00 4/15 uku. 32

Upaji Wenye Thamani Machoni pa Yehova

Ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova nchini Msumbiji ilipokea barua ifuatayo:

“Mimi ni mvulana mwenye umri wa miaka saba. Ningali katika shule ya msingi. Nawatumia fedha hizi nilizopata kwa kufuga kifaranga mmoja. Nilimwuza kwa Meticais 12,000 [dola 1 ya Marekani]. Namshukuru Yehova kwa kuwezesha kifaranga wa kwanza ambaye nimepata kufuga akue na kuwa jogoo. Ningependa mtumie zawadi yangu kwa kazi ya Ufalme wa Yehova.

“Nyongeza: Babangu alinisaidia kuandika barua hii.”

Watu wengine hufikiri kwamba ukarimu huonyeshwa tu na watu ambao wana vitu vingi vya kimwili. Lakini tunaposoma simulizi la Biblia la mjane aliyetumbukiza kwenye sanduku la hazina “sarafu ndogo mbili za thamani ndogo sana,” tunaweza kung’amua kwamba ukarimu hauonyeshwi na wingi bali huonyeshwa na nia nzuri ya moyo.—Luka 21:1-4.

Yehova huthamini kila zawadi itolewayo kwa moyo unaochochewa na upendo, hata zawadi hiyo iwe ndogo kadiri gani. Naye huwabariki sana wale wanaoiga ukarimu wake kwa kutumia wakati wao, nguvu zao, au mali zao kwa ajili ya Ufalme wake.—Mathayo 6:33; Waebrania 6:10.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki