Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w00 5/1 uku. 32
  • Alikufa kwa Sababu ya Kushikilia Kanuni

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Alikufa kwa Sababu ya Kushikilia Kanuni
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
w00 5/1 uku. 32

Alikufa kwa Sababu ya Kushikilia Kanuni

“TWAMKUMBUKA August Dickmann (alizaliwa 1910), mmoja wa Mashahidi wa Yehova.” Ndivyo yanavyoanza maneno yanayopatikana kwenye bamba moja (linaloonekana hapa) ambalo hivi majuzi lilifunuliwa katika ile iliyokuwa kambi ya mateso ya Sachsenhausen. Kwa nini mmoja wa Mashahidi wa Yehova alistahili kutajwa kwenye bamba kama hilo? Maneno yanayofuata yasimulia: “Alipigwa risasi hadharani na askari wa SS mnamo Septemba 15, 1939, kwa kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri yake.”

August Dickmann alifungwa katika kambi ya mateso ya Sachsenhausen mwaka wa 1937. Siku tatu baada ya Vita ya Ulimwengu ya Pili kuanza mnamo mwaka wa 1939, aliamriwa atie sahihi hati ya kumsajili jeshini. Alipokataa, kamanda wa kambi hiyo aliwasiliana na Heinrich Himmler, mkuu wa askari wa SS (Schutzstaffel, kikosi maalumu cha Hitler), akaomba ruhusa ya kumwua Dickmann mbele ya wafungwa wengine wote katika kambi hiyo. Septemba 17, 1939, gazeti la The New York Times liliripoti hivi kutoka Ujerumani: “August Dickmann, mwenye umri wa miaka 29, . . . ameuawa kwa kupigwa risasi na askari.” Gazeti hilo lilisema kwamba yeye ndiye Mjerumani wa kwanza kukataa kujiunga na vita kwa sababu ya dhamiri yake.

Miaka 60 baadaye, Septemba 18, 1999, kifo cha Dickmann kiliadhimishwa na shirika liitwalo Wakfu wa Ukumbusho wa Brandenburg, na sasa bamba hilo la kumbukumbu linawakumbusha watu wanaozuru mahali hapo ujasiri wake na imani yake yenye nguvu. Bamba jingine lililo kwenye ukuta wa nje wa kambi hiyo ya zamani huwakumbusha watu wanaozuru kwamba Dickmann alikuwa mmoja tu kati ya Mashahidi wa Yehova wapatao 900 walioteseka katika Sachsenhausen kwa sababu ya itikadi zao. Wengine wengi waliteseka katika kambi nyinginezo. Ndiyo, hata katika hali zenye kuogofya za kambi za mateso, wengi walishikilia kwa uaminifu kanuni za Mungu.

Kwa maoni ya Mashahidi wa Yehova, ni wajibu wa Mkristo kuwa “katika ujitiisho kwa mamlaka [serikali] zilizo kubwa.” (Waroma 13:1) Lakini, serikali zinapojaribu kuwalazimisha kukiuka sheria za Mungu, wao hufuata mfano wa mitume wa Kristo, waliosema: “Lazima sisi tumtii Mungu kuwa mtawala kuliko wanadamu.” (Matendo 5:29) Matokeo ni kwamba katika ulimwengu ambamo uadui na chuki za kikabila zimesababisha ukatili unaoshtua sana, popote walipo Mashahidi wa Yehova hufuatia amani, kama August Dickmann. Wao hufuata himizo hili la Biblia: “Usijiache mwenyewe ushindwe na lililo ovu, bali fuliza kushinda lililo ovu kwa lililo jema.”—Waroma 12:21.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki