Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w00 5/15 uku. 32
  • Wazazi Wapinga Ubaguzi wa Mwalimu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wazazi Wapinga Ubaguzi wa Mwalimu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
w00 5/15 uku. 32

Wazazi Wapinga Ubaguzi wa Mwalimu

Mwalimu wa shule ya msingi huko Cassano Murge, Italia, aliwapa baadhi ya wanafunzi wake vibandiko waende navyo nyumbani. Vibandiko hivyo, vilivyokusudiwa kubandikwa kwenye mlango wa mbele, viliandikwa hivi: “Sisi ni Wakatoliki. Mashahidi wa Yehova waagizwa wasiubishe mlango huu.”

Baadhi ya wazazi wa wanafunzi hao, ingawa wao wenyewe si Mashahidi wa Yehova, walipinga vikali matendo ya mwalimu huyo. Kulingana na jarida la habari liitwalo Muoviti Muoviti, wazazi walidai kwamba ‘kuwapa watoto ujumbe wa aina hiyo huwafanya wamkatae mtu yeyote mwenye maoni tofauti au wamtenge mtu kwa sababu eti ni “tofauti” kidini.’ Mzazi mmoja aliyeliandikia jarida hilo alikiita kibandiko hicho “mbegu ya fitina, tokeo la ujinga na upumbavu.”

Kama vile ripoti hiyo ionyeshavyo, watu wengi wasio na ubaguzi hutambua hatari za kupanda mbegu za ubaguzi. Wao pia huheshimu huduma ya Kikristo inayofanywa na Mashahidi wa Yehova kotekote nchini Italia na katika ulimwengu wote. Mbona usichukue hatua ya kuwauliza Mashahidi ‘sababu ya tumaini walilo nalo’? Watafurahi kujadiliana nawe, wakifanya hivyo kwa “staha yenye kina kirefu.”—1 Petro 3:15.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki