Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w00 9/1 uku. 32
  • Kimya Kinapokuwa Dalili ya Kukubali

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kimya Kinapokuwa Dalili ya Kukubali
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
w00 9/1 uku. 32

Kimya Kinapokuwa Dalili ya Kukubali

KITABU Betrayal—German Churches and the Holocaust chazungumzia kwa unyofu jinsi dini ilivyohusika na Utawala wa Nazi. “Wakristo wengi waliunga mkono utawala huo,” kitabu hicho chasisitiza, “na wengi wao hawakupinga hata kidogo mnyanyaso wa Wayahudi. Kimya hicho kikawa wazi.”

Ni nini katika Utawala wa Nazi kilichowavutia wale waliodai kuwa Wakristo? Kitabu hicho chaeleza kwamba wengi walishawishiwa na “hatua za kuleta utaratibu na utengamano katika jamii ya Ujerumani,” za Hitler. Chasema hivi: “Alipinga ponografia, umalaya, kutoa mimba, ugoni-jinsia-moja, na ‘upotovu’ wa sanaa ya kisasa, na aliwatuza wanawake waliozaa watoto wanne, sita au wanane kwa kuwapa nishani ya shaba, fedha au dhahabu, hivyo akiwatia moyo wadumu katika kazi yao ya nyumbani. Kupendezwa huko na maisha ya kidesturi, pamoja na uzalendo wenye kutumainia nguvu za kijeshi ambao Hitler alipendekeza kwa kusudi la kuondoa fedheha iliyopata taifa hilo iliyosababishwa na Mkataba ya Versailles, kulifanya Utawala wa Nazi uvutie wengi, hata Wakristo wengi, Ujerumani.”

Kikundi kimoja kilikuwa tofauti kabisa. “Mashahidi wa Yehova walikataa kushiriki ujeuri au kupigana vita,” chasema Betrayal. Kukataa huko kulisababisha kikundi hicho kishambuliwe kikatili, na washiriki wengi wa kikundi hicho walifungwa katika kambi za mateso. Hata hivyo, wengine waliodai kuwa ni wafuasi wa Kristo hawakupinga. Kitabu hicho chaongezea kusema hivi: “Wakatoliki na Waprotestanti kwa ujumla walionyesha uhasama wala si huruma kwa Mashahidi wa Yehova, nao walikuwa na mitazamo mikatili kama ya Hitler wala si kama ya Mashahidi wanaopinga vita.” Bila shaka, kimya kilisababisha Mashahidi watendwe vibaya zaidi chini ya utawala wa Nazi.

Huku kujihusisha kwa makanisa katika siasa za Nazi kukiendelea kubishaniwa vikali, kitabu Betrayal chasema kwamba Mashahidi wa Yehova ni “dini iliyokataa kuidhinisha au kuunga mkono utawala huo.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki